Home Mchanganyiko WAFANYABIASHARA MKOANI ARUSHA WAMLILIA HAYATI RAIS MAGUFULI

WAFANYABIASHARA MKOANI ARUSHA WAMLILIA HAYATI RAIS MAGUFULI

0
Mmoja wa wafanyabiashara mkoani Arusha Mustafa Janoowalla akisaini kitabu Cha maombolezo katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Arusha
……………………………………………………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.

Arusha.Wafanyabiashara mbalimbali mkoani Arusha ,wamemlilia aliyekuwa Rais Hayati John Magufuli kwa msiba mkubwa  ambao umekuwa ni pengo kubwa  kwa Taifa na Afrika kwa jumla.

Mmoja wa wafanyabiashara hao,Mustafa Janoowalla  kutoka kampuni ya  Royal Safety iliyopo mjini hapa alisema kuwa,Hayati Rais Magufuli alikuwa akipambania maslahi ya wananchi  bila kujali kabila lolote kikubwa ni kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mtu.
“kwa kweli msiba huu umetushtua  sana ,kwani alikuwa kiongozi  mchapa kazi na mwenye kubeba maono sana sio  kwa Tanzania  tu bali  hata kwa Afrika nzima kwa kweli tutamkumbuka kwa mambo mengi Sana Rais wetu.”alisema .

Mustafa alisema kuwa,Rais Magufuli atakumbukwa kwa maswala mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya  ikiwemo kuleta ndege ya ATCL ambayo kama nchi tunajivunia uwepo wa ndege zetu wenyewe kuliko kutegemea uwepo wa ndege kutoka nchi zetu.

Mustafa alisema kuwa,Hayati Rais Magufuli alipambana Sana kuhakikisha anakuza  sekta ya biashara ,elimu ,na afya pamoja na miundombinu pamoja  na kutengeneza barabara kila  mahali.
Naye Balozi mdogo wa Burundi hapa Arusha, Leonidas Mbakenga alisema kuwa,watamuenzi Hayati Rais Magufuli kwa namna ambavyo aliweka nchi pazuri Sana na kuibadilisha katika sekta mbalimbali.
“nilipopata taarifa nilishtuka  sana sikuamini kama Rais alitutoka   maana  nilibahatika kukaa Tanzania  kwa muda na Sasa hivi Tanzania  imebadilika sana,uchumi umeinuka sana nikafurahi Tanzania imepata kiongozi ambaye  lengo lake lilikuwa uchumi wa Tanzania  kuimarika ,pia kwa maswala ya ujirani  mwema ulikuwa vizuri sana ,  kati ya Tanzania na Burundi.”alisema.
Mbakenga alisema kuwa,kuna miradi katika serikali ya Hayati Rais Magufuli ambapo  kulikuwepo na mpango wa kujenga reli ambapo alikuwa anaboresha mambo ya usafiri Sana hivyo  waafrika wanaomboleza wote hakuna aliyetegemea kifo kama hicho kitatokea.
Alisema kuwa,Rais mpya  mama Samia Suluhu Hassan ajipe moyo maana mipango yote ya serikali  walikuwa wanafanya pamoja miradi aliyokuwa anafanya Hayati  Rais  Magufuli ataweza kuifanya na kuiboresha ili watanzania waendelee kuwa na matumaini ya kwamba huko mbele ni kuzuri.