Mmoja wa wafanyabiashara mkoani Arusha Mustafa Janoowalla akisaini kitabu Cha maombolezo katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Arusha
……………………………………………………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Wafanyabiashara mbalimbali mkoani Arusha ,wamemlilia aliyekuwa Rais Hayati John Magufuli kwa msiba mkubwa ambao umekuwa ni pengo kubwa kwa Taifa na Afrika kwa jumla.
Mmoja wa wafanyabiashara hao,Mustafa Janoowalla kutoka kampuni ya Royal Safety iliyopo mjini hapa alisema kuwa,Hayati Rais Magufuli alikuwa akipambania maslahi ya wananchi bila kujali kabila lolote kikubwa ni kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mtu.
“kwa kweli msiba huu umetushtua sana ,kwani alikuwa kiongozi mchapa kazi na mwenye kubeba maono sana sio kwa Tanzania tu bali hata kwa Afrika nzima kwa kweli tutamkumbuka kwa mambo mengi Sana Rais wetu.”alisema .
Mustafa alisema kuwa,Rais Magufuli atakumbukwa kwa maswala mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya ikiwemo kuleta ndege ya ATCL ambayo kama nchi tunajivunia uwepo wa ndege zetu wenyewe kuliko kutegemea uwepo wa ndege kutoka nchi zetu.
Mustafa alisema kuwa,Hayati Rais Magufuli alipambana Sana kuhakikisha anakuza sekta ya biashara ,elimu ,na afya pamoja na miundombinu pamoja na kutengeneza barabara kila mahali.
Naye Balozi mdogo wa Burundi hapa Arusha, Leonidas Mbakenga alisema kuwa,watamuenzi Hayati Rais Magufuli kwa namna ambavyo aliweka nchi pazuri Sana na kuibadilisha katika sekta mbalimbali.
“nilipopata taarifa nilishtuka sana sikuamini kama Rais alitutoka maana nilibahatika kukaa Tanzania kwa muda na Sasa hivi Tanzania imebadilika sana,uchumi umeinuka sana nikafurahi Tanzania imepata kiongozi ambaye lengo lake lilikuwa uchumi wa Tanzania kuimarika ,pia kwa maswala ya ujirani mwema ulikuwa vizuri sana , kati ya Tanzania na Burundi.”alisema.
Mbakenga alisema kuwa,kuna miradi katika serikali ya Hayati Rais Magufuli ambapo kulikuwepo na mpango wa kujenga reli ambapo alikuwa anaboresha mambo ya usafiri Sana hivyo waafrika wanaomboleza wote hakuna aliyetegemea kifo kama hicho kitatokea.
Alisema kuwa,Rais mpya mama Samia Suluhu Hassan ajipe moyo maana mipango yote ya serikali walikuwa wanafanya pamoja miradi aliyokuwa anafanya Hayati Rais Magufuli ataweza kuifanya na kuiboresha ili watanzania waendelee kuwa na matumaini ya kwamba huko mbele ni kuzuri.