Home Mchanganyiko SIDO, A to Z TUMEMPOTEZA KIONGOZI ALIYEFANIKISHA SEKTA YA VIWANDA

SIDO, A to Z TUMEMPOTEZA KIONGOZI ALIYEFANIKISHA SEKTA YA VIWANDA

0
Meneja wa SIDO mkoa wa Arusha Nina Nchimbi akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya mkuu wa mkoa Arusha.
Meneja masoko ya nchi za nje Silvester Kazi,kutoka katika kiwanda cha A to Z Textile Mills LTD.
………………………………………………………………………………………………
NA NANAMNYAK KIVUYO,ARUSHA.
Shirika la viwanda vidogo (SIDO)mkoa wa Arusha pamoja na kiwanda cha A to Z Textile Mills Ltd wamesema kuwa Hayati Rais Dkt John Magufuli ni kiongozi aliyefanikisha Sekta ya viwanda kwa kuwapa fursa na kutatua changamoto zilizokuwepo ikiwemo suala  umeme ambapo wanatarajia baada ya matengenezo yaliyopo hivi sasa tatizo hilo litaondoka kanisa.
Akizungumza na waandishi wa habari  Meneja wa SIDO Mkoa wa Arusha Bi.Nina Nchimbi alisema kuwa ni masikitiko makubwa mkumpoteza kiingozi jasiri na shupavu ambaye amewafikisha katika mafanikio upande wa sekta ya viwanda.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa kwani alitusaidia sana kuwezesha kuwepo kwa viwanda nakutupa miongozo kwamba inawezekana,lakini ametuachia urithi,ametuachia ujasiri na maneno ambayo sisi kama watanzania kuweza kuyaishi kufikia Tanzania ya mafanikio”.Alisema Bi.Nina
Bi.Nchimbi alisema kuwa waenzi na kuyaishi yale ambayo alikuqa akiyatarajia hayati Dkt.Magufuli hasa katika Tanzania ya viwanda kwasababu aliweza kuinua sekta ya viwanda na kufanya viwanda kuweza kuwepo huku akiwapa miongozo itakayowawezesha kuifikia Tanzania ya mafanikio na ya Viwanda.
Aidha Bi.Nina alimpongeza Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya sita ambapo atayaongoza na kuyatekeleza ba kuyakamilisha yale aliuoyaacha hayati Dkt.Magufuli akiwa kama mama.
“Nampongeza Mhe.Rais kwa kauli yake aliyowaambia watanzania kuwa yeye ni mama,ni mlezi,ni kiongozi,ni mtengeneza viongozi na muonyesha njia.”Alisisitiza Bi.Nina
Kwa upande mwingine Meneja masoko ya nchi za nje Silvester Kazi,kutoka katika kiwanda cha A to Z alisema kuwa alimfahamu hayati Dkt.Magufuli tangu akiwa Waziri wa Ujenzi ambapo katika kipindi chake cha uongozi aliweza kukusanya mapato ya nchi na kuweka nidhamu ya kuyasimamia na kuyatumia kwa faida ya watanzania.
Aidha alisema kuwa mara zote hayati Dkt.Magufuli amekuwa akiwahimiza watanzania kufanya kazi kwa pamoja ambapo aliweza kuboresha shule za kata na kuzifanya kuwa shule za mfano kwa ubira wa majeno na elimu pia inayotolewa,ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo mradi mkubwa wa maji wa bilioni 15.
“Yapo mengine ambayo pengine alikuwa hajatuonyesha yalikuwa kwenye kichwa chake na kwenye moyo wake alitamani yafanyike hatujui ni mambo gani,kwahiyo kifo chake kimetunyima mambo mengi sana kwanza yale ambayo tayari tumeshayaona bado hayajamalizika tunaamini yataendelea lakini yapo yale ambayo alipanga kuwafanyia watanzania hasa wa kipato cha chini tunaamini yataendelezwa.”alisema Kazi
Aliongeza kuwa Tanzania aliyokuwa akiifikiria hayati Dkt.Magufuli bado watanzania hawajaiona kwani nia na matamanio yake ni kuona ilikuwa ni kuona watanzania wakiwa katika viwango vya juu kiuchimi na kimaendeleo ambapo kwa muda mfupi aliokaa madarakani ameweza kupandua bandari,ujenzi wa vituo vya forodha kwenye mipaka ya nchi pamoja na ukusanyaji wa mapato na kuweka nidhamu ya matumizi.
Kazi alieleza kuwa kama watu wa viwanda watamkumbuka hayati Dkt.Magufuli kwa kufanikisha kuondoa tatizo la umeme kupitia mradi mkubwa wa umeme ambao mwakani utaweza kukamilika ambapo wanategemea kuona Tanzania katika uchumi wa kati na katika uchumi wa juu zaidi.