Mfanyabiashara wa Madini Faisal Juma shabahi akiongea na waandishi wa habari.
Mfanyabiashara wa Madini Faisal Juma shabahi akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
…………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Mfanyabiashara wa madini mkoani Arusha Faisal Juma Shabahi amesema kuwa Hayati Rais Dkt John Magufulia amewaachia watanzania na waafrika wote kwa ujumla fikra na mtazamo ambao utawafanya wawe jasiri na wazaledo.
Faisal aliyasema hayo baada ya kusaini kitabu cha maombolezo kilichopo katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo alisema kuwa kilicho fariki ni mwili na kitakachozikwa ni mwili lakini amewaachia fikra na mtazamo utakaofanya wafikie yale yote yatayo waendeleza kiuchumi.
“Fikra na mtazamo aliotuachia sisi kama watanzania ya kwamba lazima tujiamini,tuwe wazalendo,tuipende nchi yetu na kufanya yote yanayowezekana ili kuhakikisha sisi kama waafrika tuaweza kujikwamua kiuchumi na kujiendeleza kimaendeleo,” Alisema Faisal.
“Tutamkumbuka sana baba yetu na tunamshukuru kwa kila alichotufanyia kwani alitufanyia kwa upendo wa wazi sana na kwa roho ya ukunjufu na bila kuwa na tamaa yoyote, tunamuombea alale salama na tutamkumbuka milele,” Aliendelea kusema.
Aidha alisema kuwa katika sekta ya madini Hayati Rais Magufuli aliwafanyia mambo makubwa sana kwasababu aliweza kuwaita wafanyabiashara wote wa madini na kuchukua changamoto zote zilizokuwa zikiwakabili na kuweza kuzitatua kwa haraka.
“Kitendo alichoweza kukifanya cha kutukusanya kupokea changamoto zetu na kuzitatua kiliweza kuipeleka sekta ya madini katika mchango mkubwa sana wa kukusanya mapato na kuleta mabadiliko ya haraka sana katika uongozi wake,” Alieleza Faisal.
Sambamba na hayo pia alisema kuwa wanaamini kuwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu atayarithi na kuyaedeleza yale yote Hayati Rais Dkt Magufuli aliyoyaazisha kwani alifanya nae kazi kwa muda mrefu na alimuelewa alichokifanya na kimsingi kabisa kuwa bado ilani ya chama cha mapibduzi ndiyo itayoendelea kuweka mikakati.