……………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Akimuaga Shujaa wa Afrika Mzalendo wa Tanzania Hayati Dkt.John Magufuli ,Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi amesema kuwa Hayati Magufuli ameboresha maisha na kujali wananchi wake,kutetea na kuendeleza uchumi.
Mhe.Tshisekedi ameyasema hayo leo Machi 22, 2020 katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma wakati wa kuaga mwili wa Magufuli.
Aidha Mhe.Tshisekedi amesema kuondoka kwake ni pigo kwa Bara la Afrika kwa kuwa ni mwanasiasa mkongwe alikuwa mpiganaji na mzalendo, mtetezi mkuu wa uhuru wa utamaduni na kiuchumi barani Afrika.
“Tutabaki na kumbukumbu ya mtu mpiganaji na mzalendo, siyo tu kwa maslahi mapana ya Tanzania bali pia kwa umoja wa Afrika,aliyekuwa analenga kutimiza ndoto ya waasisi wa mataifa yetu uliolenga kuleta umoja kwa Afrika na baina ya mataifa yetu.”amesisitiza Tshisekedi
Hata hivyo amesema kuwa Mhe.Dkt.Magufuli siku zote alitamani kuona maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanayotekelezwa na Waafrika kwa niaba ya Waafrika na Watanzania kwa ujumla hivyo Rais wa Tanzania wimbi lililosababishwa na kifo cha Magufuli haitakiwi kamwe kupunguza dhamira yenu na nia yenu kuendeleza dira na dhima aliyokuwa nayo Magufuli.
“Hii ni fursa kwenu kuja pamoja na kutimiza ndoto inayolenga kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Tanzania. tunaoongelea dhamira na dhima yake ninapenda kutaja kati ya mengi tu mapambano aliyoyaendesha dhidi ya ubadhirifu wa mali, fedha na rushwa ambayo ni kansa iliyokuwa inatafuna na kuchelewesha maendeleo ya bara la Afrika.”Amesema.
Hafla ya kumuaga Hayati Dkt.John Magufuli kitaifa imefanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassana pamoja na Marais wa nchi zaidi ya 10 na viongozi mbalimbali kutoka nje ya Tanzania wamehudhuria tukio la kutoa heshima za mwisho.