Home Mchanganyiko MBUNGE WA LUPA MASACHE KASAKA ASHIRIKI KUAGA MWILI WA HAYATI DK. MAGUFULI...

MBUNGE WA LUPA MASACHE KASAKA ASHIRIKI KUAGA MWILI WA HAYATI DK. MAGUFULI VIWANJA VYA BUNGE

0

Mbunge wa Jimbo la Lupa Mheshimiwa Masache Kasaka akitia saini kitabu cha Maombolezo ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Magufuli Bungeni Dodoma leo asubuhi.

Buriani Baba, Kwaheri Kiongozi Wetu Kwa heri shujaa wetu, ndivyo anavyoonekana kusema katika moyo wake Mh. Masache Kasaka.

Mheshimiwa Masache ameungana na wabunge wengine kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli ambaye mwili wake umefikishwa bungeni na wabunge kutoa heshima zao za mwisho.

Mbunge wa jimbo la Lupa Mheshimiwa Masache Kasaka amemuelezea Hayati Magufuli kuwa alikuwa kiongozi shupavu aliyeongoza Taifa kwa ujasiri na Uthubutu ambaye alionesha mapenzi yake dhahiri kwa Watanzania.

Mbunge wa jimbo la Lupa Mheshimiwa Masache Kasaka wa pili kutoka kulia mstari wa nyuma waliokaa akiwa pamoja na waheshimiwa wabunge wengine wakisubiri kuaga mwili wa Hayati Dk John Pombe Magufuli kwenye viwanja vya Bunge leo jijini Dodoma

Mheshimiwa Masache Kasaka akiwa katika picha pamoja na baadhi ya wabunge.