Home Siasa KIKAO CHA DHARURA CHA KAMATI KUU YA CCM CHAFANYIKA LEO JIJINI DAR...

KIKAO CHA DHARURA CHA KAMATI KUU YA CCM CHAFANYIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM, KUFUATIA KIFO CHA DK. MAGUFULI

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Ukumbi tayari kushiriki Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.  Kikao hicho kimefanyika kwa dharura kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk. John Magufuli kufariki dunia Machi 17, 2021. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete ambaye pia amehudhuria kikao hicho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi wakiwa katika Ukumbi tayari kushiriki Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.  Kikao hicho kimefanyika kwa dharura kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk. John Magufuli kufariki dunia Machi 17, 2021. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi wakipitia makabrasha kabla ya kuanza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.  Kikao hicho kimefanyika kwa dharura kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk. John Magufuli kufariki Dunia Machi 17, 2021.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibara Dk. Ali Mohamed Shein na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa wakiwasili ukumbini kwenye kikao hicho

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akitoa utangulizi wa kuanza kwa kikao hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akitoa utangulizi wa kuanza kwa kikao hicho

Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akiwa kwenye kikao hicho. Wapili ni Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume.

Wajumbe wakiwa ukumbini kwenye kikao hicho. Mbele ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Pereira Silima na kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.

Wajumbe wakiwa Ukumbini kwenye kikao hicho. Baadhi yao Mbele ni Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda

Maafisa Waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu wakiwa kwenye kikao hicho. Kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi Ndugu Mwansasu.

Wajumbe waakiwa Ukumbini kwenye kikao hicho. Baadhi yao Mbele -Kulia ni Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa na nyuma yake ni Spika wa Bunge Job Ndugai.

Wajumbe Dk. Jakaya Kikwete na Amani Abeid Karume wakipitia makabrasha wakati wa kikao hicho. Nyuma yao ni Dk. John Mndolwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Herry James akipitia makabrasha wakati wa kikao hicho

Wajumbe wakiendelea kufuatia mazungumzo mbalimbali kwenye kikao hicho.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Makongoro Nyerere akifuatili katika makabrasha wakati wa kikao hicho