Jengo la maabara ya TMDA lililopo Nyakato Buzuruga, Mwanza
Mwenyekiti wa MAB, Bw. Erick Shitindi akiwasilisha taarifa mbele ya Kamati
Mkurugenzi wa Huduma za Maabara, Dkt. Danstan Hipolite akieleza jambo kwa kamati ya Bunge ndani ya Maabara ya TMDA
Ukaguzi wa jengo la TMDA ukiendelea
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Mitangu Fimbo akieleza jambo kwa Wajumbe wa kamati ndani ya Maabara ya TMDA
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma, Mhe. Mwakibete akiongoza wajumbe kukagua mradi wa jengo la Maabara ya TMDA jijini Mwanza
…………………………………..
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji wa Umma ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Atupele Mwakibete imeipongeza TMDA kwa utekelezaji mzuri wa Mradi wa ujenzi wa Maabara ya Kisasa Jijini Mwanza
Mhe. Mwakibete amesema hayo tarehe 17 Machi, 2021 mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa jengo la TMDA pamoja na Maabara ya uhakiki wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba.
“Kamati imeridhika na utekelezaji wa mradi huu na kwamba thamani ya fedha iliyowekwa na Serikali inaonekana”
Mhe. Mwakibete alisema kuwa vifaa vya kisasa vilivyowekwa katika maabara hii na kama walivyojionea ni ushahidi tosha wa Mamlaka imejipanga na kujikita katika kulinda Afya ya jamii kupitia mradi huu.
Kamati imeitaka TMDA kuweka mikakati ya kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wake katika kufanya marekebisho ya machine na mitambo iliyowekezwa katika maabara hii badala ya kutegemea mafundi toka nje ya nchi.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Bw. Erick Shitindi, wakati akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa mradi huo mbele ya Kamati alisema kuwa lengo ujenzi wa ofisi na maabara ya TMDA katika Kanda ya ziwa ni kusogeza huduma za udhibiti karibu zaidi na wananchi ikiwa ni pamoja na maabara hiyo kuhudumia nchi jirani na Tanzania.
Maabara ya TMDA kanda ya Ziwa ina machine na mitambo ya kisasa yenye thamani ya takriban TZS 5 bilioni.