Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Nchini Dkt Maduhu Kazi akizungumza na waandishi wa habari leo March 17,2021 jijini Dodoma baada ya kikao kilichowakutanisha wadau wa uwekezaji na Wizara za kisekta kilicholenga kuibua na kushirikishana fulsa zilizopo katika mradi wa SGR.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa akizungumza na wanahabari leo March 17,2021 jijini Dodoma mara baada ya kikao kilichowakutanisha wadau wa uwekezaji na Wizara za kisekta kilicholenga kuibua na kushirikishana fulsa zilizopo katika mradi wa SGR.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Nchini TIC Dkt Maduhu Kazi akiongoza kikao kilichowakutanisha wadau wa uwekezaji na Wizara za kisekta kilicholenga kuibua na kushirikishana fursa zilizopo katika mradi wa SGR.
……………………………………………………………………………
Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.
Kituo cha uwekezaji hapa nchini TIC kimewakutanisha wadau wa uwekezaji pamoja na Wizara za kisekta katika uwekezaji ili kwa pamoja kubaini na kushirikishana fursa zilizopo katika mradi wa reli ya kisasa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho Mkurugenzi wa TIC Dkt Maduhu Kazi amesema lengo ni kuzitambua fulsa zilizopo ili kuinua uchumi wa nchi na mradi huo uweze kuleta tija.
Dkt Maduhu Kazi amesema hadi hivi sasa jumla ya miradi ya uwekezaji 30, imeibuliwa kwenye maeneo ambayo reli ya kisasa (SGR) imepita na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo.
Pia amebainisha kuwa baadhi ya fursa za miradi hiyo ya uwekezaji iliyoibuliwa ni pamoja na Matangazao, Kilimo, Hoteli, Viwanda, Migahawa pamoja na uwekezaji katika taasisi za kifedha.
Aidha amesema toka Septemba mwaka jana kituo cha uwekezaji nchini, kwa kushirikina na taasisi mbalimbali za serikali wamekuwa na mchakato wa kutafuta na kuibua fursa zilizopo kwenye mradi wa SGR.
“Miradi hii ni ile ambayo itaongeza shughuli za usafirishaji katika njia hii ya reli na siyo kutegemea abiria pekee yao hivyo basi miradi kama ya kilimo itatoa malighafi nyingi ambazo zitahijita kusafirishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine”amesema.
Dkt Maduhu amesema kuwa, kati ya miradi 30 ni miradi 14 ambayo ndiyo imeshakamilika kwajili ya kufanyiwa uwekezaji hivyo wameona ni muhimu sasa kukutana na sekta binafsi ili kuiuza.
Ameongeza kuwa “Leo hii katika kikao hiki pia tumewaita wenzetu wa sekta binafsi ambao wametupa mawazo mazuri sana katika miradi hii ambayo tumeiibua na baadaye wataalam wataiweka vizuri na tutaandaa kitabu ambacho kitatumia kuiuza kwa wawekezaji pamoja na kwenye tovuti yetu” amesema.
Pia Dkt. Maduhu amesema kuwa miradi hiyo itakuwa ni kwajili ya kipande cha Dar es saalam hadi Morogoro na baadaye wataendelea kuibua fursa nyingine kulinga na ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR utakavyokuwa unakamlika ikiwamo kutoka Morogoro hadi Dodoma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa, amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kukutana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanapata wawekezaji katika maeneo ambayo reli ya SGR inapita.
“Hili ni agizo la mweshimiwa Rais Magufuli, alilolitoa alipotembelea mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa na kututaka kuhakikisha kuwa katika maeneo ambayo reli imepita kunawepo na shughuli mbalimbali za uwekezaji ili kuchochea utendaji wa shirika” amesema Kadogosa.
Mwakilishi kutoka Taasisi ya sekta binafasi (TPSF) Kenned Rwehumbiza, amesema wameshiriki katika kikao hicho ili kuweza kuzitambua fursa za uwekezaji zilizopo katika mradi wa reli ya kisasa SGR na kuzifikisha kwa wananchi.
“Lakini kazi yetu kubwa ni kuangalia namna gani tunaweza kuzikama hizi fursa na kuzipeleka kwa wananchi ili waweze kuzifanyia kazai kwani tunaelezwa kuwa kuanazia Agosti mosi mwaka huu safari za Dar Moro zitaanza”amesema.