Home Mchanganyiko KAMATI YA MIUNDOMBINU YAMPONGEZA RAIS DK. MAGUFULI UJENZI WA DARAJA LA SALENDER

KAMATI YA MIUNDOMBINU YAMPONGEZA RAIS DK. MAGUFULI UJENZI WA DARAJA LA SALENDER

0

  

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati kamati hiyo ilipotembelea ujenzi wa darajala Salender Dar es salaam kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Seleman Moshi Kakoso.

Mtendaji mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale akiuelezea mradi  wa Daraja jipya la Selander utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 243.7, unatekelezwa na Kampuni ya GS Engineering Corporation kutoka Korea Kusini mbele ya wajumbe wa kamati ya Miundombinu kulia Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya.

Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Miundombinu wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale hayupo pichani.

Mhandisi wa Daraja, Mwanamama  Lulu Dunia kutoka Kampuni ya Afrisa Consulting, ya Dar es salaam akitoa maelezo ya ujenzi wa daraja hilo kwa wajumbe wa kamati hiyo.

Picha zikionesha baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakifuatilia uwasilishajiwa maelezo kutoka kwa wataalamu wa TANROADS.

Mhandisi wa Daraja, Mwanamama  Lulu Dunia kutoka Kampuni ya Afrisa Consulting, ya Dar es salaam akitoa maelezo ya ujenzi wa daraja hilo kwa wajumbe wa kamati hiyo.

Baadhi ya nguzo za daraja hilo la Salender zikiendelea kujengwa kama zinavyoonekana.

Kutoka kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Seleman Moshi Kakoso, Makamu Mwenyekiti Mama Anne Kilango Malecela na baadhi ya wajumbe wakisikiliza wakati majumuisho ya ziara hiyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya akiwashukuru wajumbe hao mara baada ya kumalizia ziara yao katika daraja hilo.

Kutoka kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Seleman Moshi Kakoso, Makamu Mwenyekiti Mama Anne Kilango Malecela na baadhi ya wajumbe wakisikiliza wakati majumuisho ya ziara hiyo.

………………………………………….

*TANROADS Yapewa tano kwa kufundisha wahandisi wanafunzi.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Seleman Moshi Kakoso amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa daraja la Salender Dar es salaam unaoendelea.

Kakoso amesema Daraja jipya la Selander litatoa ufumbuzi mkubwa wa foleni ya magari katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar es Salaam na kuondoa adha ya watumiaji kwa kiwango kikubwa.

“Ninampongeza sana Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli kwa kuanzia kutekeleza mradi huu mkubwa wa Daraja jipya la Selander,” amesema.

Ameongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mheshimiwa Mh. Seleman Kakoso kuwa daraja hilo litatoa ufumbuzi mkubwa wa foleni kwenye barabara ya Ali Hassan Mwinyi, TANROADS mmeandika historia kubwa sana nchini kwa kazi hii, 

Mheshimiwa Kakoso ametoa kauli hiyo leo Machi 17,2021 wakati Kamati ya Miundombinu ilipotembelea Daraja  la Selander ambalo ujenzi wake unaendelea  baada ya kupata taarifa za ujenzi kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale.

Amewataka TANROADS kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa na kuweka  mfumo wa ulinzi kwa ajili ya usalama wa miundombinu ya daraja hilo.

Mheshimiwa Kakoso amesema Kamati yake imefurahishwa na mpango wa Serikali wa kuweka utaratibu maalum wa kuwafundisha vijana wanaotoka vyuoni.

Akitoa maelezo kwa kamati hiyo Mtendaji mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mfugale amesema mradi wa Daraja jipya la Selander utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 243.7, unatekelezwa na Kampuni ya GS Engineering Corporation kutoka Korea Kusini.

Ameongeza kuwa mradi huo unaendelea kutoa mafunzo kwa wahandisi Wanawake kutoka taasisi mbalimbali, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Wahandisi wahitimu (aGraduate trainees) 16, tunategemea mafunzo haya yatasaidia kujenga uwezo na ujuzu utakaosaidia Taifa hapo baadaye.

“Mradi wa Daraja jipya la Selander umeajiri wafanyakazi 962, kati yao asilimia 92 ni wazawa wakiwemo wataalam na wafanyakazi wa kawaida na asilimia nane ni wataalam kutoka nje ya Tanzania,”. Amesema Mfugale.

Naye Mhandisi wa Daraja, Mwanamama Lulu Dunia kutoka Kampuni ya Afrisa Consulting, ya Dar es salaam amesema ujenzi wa daraja umefikia asilimia 71.3, unategemewa kukamilika kwa wakati.