*******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kuichapa Al Merrikh ya Sudan mabao 3-0 katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika .
Simba ilianza kupata bao dakika dakika 18 kupitia kwa nyota wao Luis Miquissone wakati bao la pili likiwekwa kimyani na beki kisiki wa pembeni Mohamed Hussien mnamo dakika ya 38.
Hadi mapumziko timu ya Simba ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-0. kipindi cha pili kilivyoanza Simba iliendelea na kasi ya kushambulia lango la mpinzani na kubahatika kupata bao la tatu kupitia kwa mshambuliaji wao Chris kope Mugalu dakika ya 49 ya mchezo.
Hadi dakika 90 matokeo yalibaki Simba Sc 3-0 Al Marrekh hivyo kuifanya Simba Sc kuongoza kundi kwa pointi 10 katika kundi lake.