Home Mchanganyiko BASHE AMALIZA MGOGORO WA ARDHI MVOMERO.

BASHE AMALIZA MGOGORO WA ARDHI MVOMERO.

0

Naibu Waziri Kilimo Mhe Hussein Bashe (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (kushoto) wakifungua Maji Kwenye mfeleji katika Skimu ya umwagiliaji ya Mvumi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kamati ya Bunge ya kudumu ya Kilimo,Mifugo na Maji ilipotembelea Mradi huo.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe akitoa maelekezo kwa Kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilomo Bwana Gerald Kusaya pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero wakati wa ziara ya kamati ya Bunge ya kudumu ya Kilimo,Mifugo na Maji.

Naibu waziri Kilimo Mhe Hussain Bashe akikagua vyoo vilivyojengwa kwenye Mradi wa Ghala la kuhifadhia Mpunga katika Skimu ya umwagiliaji ya Kigugu Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro akiwa ameambatana na Kamati ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji(kushoto) ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt Cristine Ishengoma, ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Morogoro,walipofika kukagua Mradi huo March 16.2020.

*****************************

Na Farida Saidy, Morogoro.

Wananchi wa vijiji vya Kigugu na mbogo Komtonga Wilayani Mvomero Mkoani Morogororo Wanaojishughulisha na kilimo cha Mpunga katika Skimu ya Umwagiliaji ya Kigugu wameshindwa kuendelea na shughuli za uzalisha wa zao hilo mara baada ya kuelezwa kuwa eneo hilo lipo chini ya Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii Jinsi wazee na watoto,Kitengo Ustawi wa jamii.

Wakulima hao wametoa kilio chao mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo ,Mifugo na Maji wakati ilipotembelea katika miradi hiyo na kukagua shughuli zinazoendelea ambapo wamekuta baadhi ya wakulima wakishindwa kuendelea na shughuli za kilimo kutokana na mgogoro huo.

Akijibu hoja hizo NAIBU waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe amewataka wakulima kuendelea kuendelea kulima katika Skimu  ya Uwagiliaji ya Kigugu kwa kuwa wizara haina taarifa juu ya suala hilo.

“Hao walikuja hapa walikuta tayari kuna mradi wa wizara ya kilimo,hivyo kungekuwa na swala la mgogoro wangekuja kwetu sisi watu wa wizara ya Kilimo ili wapate ufafanuzi zaidi.”.Alisema Mhe Bashe

Hata hivyo Naibu waziri Bashe ameitaka serikali ya Halmashuari ya Wilaya ya Mvomero kupima eneo hilo lenye hakari mia nane na kutolewa kwa wananchi wa vijiji hivyo ili waendeleze shughuli za uzalishaji wa zao la Mpunga Kama lilivyopangwa na Serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dakta Christine Ishengoma ameitaka wizara kilimo kuhakikisha inashirikiana haraka na wizara ya afya ili kumaliza sitofahamu hiyo ili wananchi kuweza kuendelea na shughuli zao za uzalisha wa mpunga kwa ufanisi Zaidi.

Kamati hiyo imetembelea miradi ya Skimu ya umwagiliaji pamoja na maghala la kuhifadhia mazao ya Mpunga katika Wilaya Mvomero na Kilosa,huku ikionyesha kulidhika na ujenzi wa miundombino ya maghala pamoja na Skimu za umwagiliaji zilizojengwa kwa ufadhili wa Bank ya dunia chini ya mradi wa kuongeza uwezo zao la mpunga nchini na kusimamiwa na wizara ya Kilimo.
Mwisho