Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, mara baada ya kutembelea mradi wa Magomeni Kota Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akiongea jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Godfrey Kasekenya wakati wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kutembelea Ujenzi wa Mradi wa Magomeni Kota leo Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Godfrey Kasekenya akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, mara baada ya kutembelea mradi wa Magomeni Kota Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Wakala wa Majengo TBA wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu mara baada ya kamati hiyo kutembelea mradi wa Magomeni Kota leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe.Selemani Kakoso akizungumza mara baada ya kamati hiyo kutembelea mradi wa Magomeni Kota leo Jijini Dar es SalaamMeneja wa Mradi wa Magomeni Kota (TBA) Bw. Benard Mayemba akizungumza mara baada ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kutembelea mradi wa Magomeni Kota leo Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi wa Barabara na Ujenzi wa Wakala wa Majengo (TBA) Ladislaus
Bigambo akiwaonyesha na kuwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Miundombinu gari lililofungwa mitambo maalum kwa ajili ya kukagua
ubora wa barabaraMajengo ya magomeni Kota ambayo yamekamilika kwa asilimia 93 ambayo pia serikali imeweza kuwekeza fedha asilimia 98 ya ujenzi huo, Ujenzi huo ulisimamiwa na Wakala wa Majengo TBA mpaka kufikia sasa.
Meneja wa Mradi wa Magomeni Kota (TBA) Bw. Benard Mayemba akielekeza jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu mara baada ya kutembelea mradi wa Magomeni Kota leo Jijini Dar es Salaam Meneja wa Mradi wa Magomeni Kota (TBA) Bw. Benard Mayemba akiwaongoza wajumbe wa kamati ya Bunge ya Miundombinu mara baada ya kutembelea mradi wa Magomeni Kota leo Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa mafundi akiendelea na shughuli yake katika ujenzi wa majengo maalumu Makomeni Kota ambayo yamekamilika kwa asilimia 93 hadi sasa.
(Picha na Emmanuel Mbatilo)
*************************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Serikali imeombwa kuwawezesha Wakala wa Majengo (TBA) kwa kutenga fedha za kutosha ili kuweza kujenga katika maeneo yaliyobaki kwani mpaka sasa wameweza kufanikisha ujenzi wa Majengo ambayo yaliyokuwa yanatakiwa kujengwa maeneo hayo ambapo mpaka sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia 93.
Ameyasema hayo leo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe.Seleman Kakoso mara baada ya kutembelea mradi wa Magomeni Kota Jijini Dar es Salaam kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Akizungumza katika eneo hilo Mhe.Kakoso amesema eneo la Magomeni Kota ni kubwa serikali ililitenga kwaajili ya makazi ya wananchi hivyo Serikali iwekeze fedha za kutosha kuweza kuongezwa kwa miradi mingine ya ujenzi katika eneo hilo.
“Mradi kama huu tunaweza kuzalisha Kariakoo nyingine maeneo kama haya kwasababu wameonesha nia ambayo mnaiona kwahiyo endapo mkiwawezesha wanaweza kufanya mambo makubwa”. Amesema Mhe.Kakoso.
Aidha Mhe.Kakoso amesema ulipwaji wa fedha kuwalipa TBA pindi wanapofanya kazi haupo hivyo wameiomba wizara iweze kusaidia TBA kupata haki na stahiki zao.
“kumekuwa na kasumba taasisi nyingi za serikali zinapopata nafasi ya kuhudumiwa na taasisi nyingine taasisi nyingine inaonewa kwahiyo kwa TBA tunaomba muwalipe haki na stahiki zao, TBA wamesimamia majengo yale ya mji mpya wa Mtumba kule Dodoma mpaka sasa hawajalipwa fedha zao tunaomba hili mkalishughulikie muwasimamie waweze kulipwa fedha ili waweze kujiendesha”. Amesema Mhe.Kakoso.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Godfrey Kasekenya ametoa rai kwa taasisi za UMMA ambazo zinadaiwa na TBA waweze kuwalipa ili wawe na uwezo wa kuendelea kujenga zaidi miundombinu ya majengo ya serikali.
Pamoja na hayo amesema kufikia mwezi Aprili mwaka huu majengo yote yatakamilika kwani kufikia hadi sasa ujenzi umeweza kukamilika kwa asilimia 93 kuweza kumalizaka
“Tunauhakika kwa mwendo tunaokwenda nao kufikia mwezi wa 4 majengo haya yatakuwa yamekamilika kwani asilimia 98 za gharama za mradi huo zimeshatolewa hivyo kufikia kipindi hicho watu watakuja kuishi hapa”. Amesema Mhe.Kasekenya.