Home Mchanganyiko ZIARA YA KAMATI YA BUNGE VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YATEMBELEA MAENEO LA...

ZIARA YA KAMATI YA BUNGE VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YATEMBELEA MAENEO LA UWEKEZAJI WA VIWANDA YALIYO CHINI YA EPZA BAGAMOYO NA UBUNGO KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.

0

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. David Mwakiposa Kihenzile(Mb) huku ikiwa imeambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe ikiendelea na ziara yake katika Maeneo Maalum ya uwekezaji kwa mauzo ya nje (EPZA) Ubungo, Dar es salaam. Machi 15, 2021

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ikiwa eneo la uwekezaji la Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) kukagua na kujionea utendaji kazi wa kiwanda African Dragon kinachozalisha malighafi za mabati ya kuezekea kwa ajari ya kuuza Kwenye viwanda Vya Mabati nchini na Nje ya nchi. Bagamoyo, Pwani. Machi 15, 2021

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Mwakiposa Kihenzile(Mb) huku wakiwa wameambatana na wajumbe wa kamati hiyo wakikagua utendaji kazi wa kiwanda cha nguo cha Took Garmet kinachotengeneza nguo aina ya jinsi na Tshirt na kimeajiri wafanyakazi Zaidi ya 3,700 kipo eneo Maalum ya uwekezaji kwa mauzo ya nje (EPZA) Ubungo, Dar es salaam. Machi 15, 2021

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ikiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe na maafisa kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembelea kiwanda cha Card Africa kinachojihusisha na utengenezaji wa kadi za benki, vocha, kadi za simu kilichopo eneo Maalum ya uwekezaji kwa mauzo ya nje (EPZA) Ubungo, Dar es salaam. Machi 15, 2021

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. David Mwakiposa Kihenzile(Mb) huku ikiwa imeambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe ikipokea taarifa za ujenzi wa kiwanda cha kuchakata nyama cha Tanfroz Ltd kilichopo eneo Maalum ya uwekezaji Bagamoyo, Pwani. Machi 15, 2021

Wafanyakazi wa kiwanda cha ha nguo cha Took Garmet kinachotengeneza nguo aina ya jinsi na Tshirt wakiendelea na kazi, kimeajiri wafanyakazi Zaidi ya 3,700 kipo eneo Maalum ya uwekezaji kwa mauzo ya nje (EPZA) Ubungo, Dar es salaam. Machi 15, 2021

Picha zote na Eliud Rwechungura.

**************************************

Na Eliud Rwechungura

Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira inaendelea na ziara zake na imetembelea Maeneo Maalum ya uwekezaji kwa mauzo ya nje (EPZA) yaliyoko Bagamoyo Mkoa wa Pwani na Ubungo Mkoa wa Dar es salaam na kukagua shughuli mbalimbali za uendelezwaji wa Viwanda.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. David Kihenjile (Mb) imetembelea eneo la uwekezaji la Bagamoyo na kutembelea ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata nyama cha Tanfroz Ltd ambacho kinaendelea na ujenzi na kiwanda cha kutengeneza mabati malighafi za mabati ya kujengea cha African Dragon.

Aidha kamati imetembelea eneo maalum la uwekezaji kwa mauzo nje (EPZA) na kutembelea kiwanda cha nguo cha Took Garmet kinachotengeneza nguo aina ya jinsi na Tshirt na kimeajiri wafanyakazi Zaidi ya 3,700. Kiwanda hiki kinazalisha nguo na kuuza katika masoko ya AGOA kwa asilimia 80 na mauzo ya ndani ya nchi ni asilimi 20.

Pia kamati imetembelea kiwanda cha Card Africa kinachojihusisha na utengenezaji wa kadi za benki, vocha, kadi za simu ambapo kamati hiyo ya kudumu ya bunge ya viwanda, biashara na mazingira imeridhishwa na kazi inayofanya na taasisi hii iliyo chini ya wizara ya Viwanda na Biashara kwa kazi nzuri wanayofanya kupitia taasisi hii ya kutengeneza mazingira bora kwa wawekezaji na kuitaka EPZA kutafuta wawekezaji na kuwapeleka katika maeneo waliyotenga ili wawekeze Viwanda vya kuchakata malighafi za ndani ili kuongeza ajira na kodi kwa serikali.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira, Mhe. David Kihenzile (Mb) amesema kuwa amefurahishwa na ujenzi wa uchumi wa viwanda katika maeneo maalum ya uwekezaji, kwani viwanda hivi vinaleta ajira nchini na kuongeza pato la taifa kwa kupata kodi. “Sisi kama kamati tutaendelea kuhamasisha Wizara ya Viwanda na Biashara kuendelea kuboresh mazingira ya uwekezaji na kufanya ziara ya kina katika viwanda hivyo na kutatua cchangamoto zinazowakabili” Amesema Kihenzile.

Naye, waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) amesema kuwa lengo kubwa la ziara hii ni kujionea miradi ya Serikali kupitia Maeneo Maalum ya uwekezaji kwa mauzo ya nje (EPZA) na kuona miradi ya kimkakati ambayo haijaanza ili kuishauri serikali namna bora ya uendelezaji wa maeneo haya ili yawe na tija kwa wananchi.

Mhe. Mwambe (Mb) amesema kuwa kamati imejionea mkazo mkubwa unaofanywa na serikali katika ujenzi wa uchumi wa Viwanda. EPZA wameandaa maeneo na wanaendelea kuandaa maeneo ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji wa Viwanda.

“kamati imejionea uwekezaji unaofanywa na EPZA na miradi mingine ya kimkakati inayokuja kutekelezwa na baada ya ziara ya kamati katika maeneo yote kamati itakuja na majumuisho ya namna bora ya uishauri serikali na sisi kama Wizara tutafanyia kazi ushauri huo ili kuifikia malengo tuliyojiwekea ya kuifanya nchi yetu kuwa ya Viwanda” Amesema Mwambe.

Kamati inaendelea na ratiba ya kutembelea maeneo ya uwekezaji na taasisi za uendelezwaji Viwanda.