Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge akikagua Miche ya Kahawa iliyopandwa na Kikosi cha 844 KJ Itende kwa maadhumuni ya kukuza zao la Kahawa leo March 15,2021.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge,akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shamba la Kahawa wa kikosi cha 844 KJ Itende Kapteni Emmanuel Mwakimage,wakati alipotembelea Shamba hilo lililopo katika kikosi hicho leo March 15,2021.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge,akimsikiliza Meneja Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bodi ya Kahawa Tanzania Bw. Sijali Bowa,wakati alipotembelea Shamba la Kahawa Mpya zililopo Katika Kikosi cha 844 KJ Itende leo March 15,2021.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge,akisisitiza jambo kwa Meneja Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bodi ya Kahawa Tanzania Bw. Sijali Bowa,wakati alipotembelea Shamba la Kahawa Mpya zililopo Katika Kikosi cha 844 KJ Itende leo March 15,2021.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge akikagua Shamba la Mahindi la ekari 100 yaliyolimwa na Kikosi cha 844 KJ Itende kwa maadhumuni ya kuzalisha Chakula ili kujitosheleza kulisha kambi za JKT leo March 15,2021.
Muonekano wa Shamba la Mahindi la ekari 100 linalolimwa na Kikosi cha 844 KJ Itende kwa maadhumuni ya kuzalisha Chakula ili kujitosheleza kulisha kambi za JKT leo March 15,2021.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukagua Shamba la Mahindi la ekari 100 linalolimwa na Kikosi cha 844 KJ Itende kwa maadhumuni ya kuzalisha Chakula ili kujitosheleza kulisha kambi za JKT leo March 15,2021.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge ,akifunua kitambaa kuashiri uzinduzi wa Bwalo la chakula la masajenti na Maafisa wateule katika Kikosi cha 844 KJ Itende,kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi JKT,Kanali Hassan Mabena leo March 15,2021.
Muonekano wa Bwalo la chakula la masajenti na Maafisa wateule katika Kikosi cha 844 KJ Itende leo March 15,2021.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge,akipanda Mti kama ishara ya uzinduzi wa Bwalo la chakula la masajenti na Maafisa wateule katika Kikosi cha 844 KJ Itende leo March 15,2021.
……………………………………………………………………………………………………………
Na Alex Sonna,Mbeya
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limepokea mbegu za kahawa kilo 300 za kuzalisha miche milioni 1 kwa ajili ya kuigawa kwa wananchi na mingine kutumia na kikosi hicho ikiwa ni mikakati ya kukuza zao hilo.
Hayo yalibainishwa leo March 15,2021 jijini Mbeya na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mazao ya kimkakati ambayo Jeshi hilo limejikita kuyaendeleza.
Amesema mbegu hizo zimetolewa na Bodi ya Kahawa ikiwa ni utekelezaji wa mkataba wa JKT na Bodi hiyo.
Meja Jenerali Mbuge amesema wamejipanga kuboresha mazao ya kimkakati likiwemo la Kahawa ili kusaidia kukuza uchumi wa taifa.
“JKT inatekeleza agizo la Rais Dk John Magufuli la kuwataka wajitegemee katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili kuepuka kutegemea fedha za serikali,”alisema Meja Jenerali Mbuge.
JKT imeweka mikakati ya kuhakikisha inaongeza uzalishaji kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi, na kwa upande wa kilimo kipaumbele kimewekwa kwenye kuzalisha mazao ya chakula ya mpunga mahindi, maharage.
Kwa upande wa mazao ya kimkakati ya kibiashara JKT imejielekeza katika kulima mazao ya Alizeti, Parachichi, Mkonge, Mchikichi na Kahawa.
Naye Meneja wa Shamba wa kikosi cha JKT Itende Kapteni Emmanuel Mwakimage alisema mkakati wa jeshi alisema kwa upande wa kahawa kikosi hicho kwa sasa kinaondoa miche ya zamani ya kupanda michezo mipya yanye ubora na mkakati ni kupanda ekari 20 kila mwaka.
Amesema kuwa kikosi kimeanza kwa kupanda ekari 50 mpya kwa kupanda miche yao ambayo inaanza kutoa matunda kwa muda wa miaka mitatu.
Naye Luteni kanali Juma Mrai amesema mbali na ekari 100 zinazolimwa katika kikosi cha Itende ikiwa ni mkakati wa kujitosheleza kwa chakula, kuanzia mwakani kiwango hicho kitaongezeka kwa kulima ekari 300 za mahindi na ekari 500 za alizeti katika eneo la Momba.
Kwa upande wake Meneja Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bodi ya Kahawa Tanzania Bw. Sijali Bowa amesema kuwa kutokana na kuangalia uzalishaji wa JKT Itende wameamua kuingia mkataba wa kzualisha michezo million moja kila mwaka kwa miaka mitano na baadhi ya michezo hiyo itagawiwa kwa jamii na mingine itabaki kikosini kwa ajili ya kuendeleza mpango wao wa kukuza zao hilo.