Home Biashara KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAFURAHISHWA NA UTENDAJI WA SHIRIKA LA MAWASILIANO...

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAFURAHISHWA NA UTENDAJI WA SHIRIKA LA MAWASILIANO TTCL

0

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile katikati akiongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mh. Suleiman Kakoso wa pili kutoka kulia wakati kamati hiyo ilipotembelea Mkongo wa mawasiliano wa  Taifa unaomilikiwa na  shirika la Mawasiliano TTCL kushoto ni Waziri Kindamba Mkurugenzi wa Shirika hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Suleiman Kakoso akihoji jambo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile wakati kamati hiyo ilipotembelea katika shirika la Mawasiliano TTCL katikati ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Waziri Kindamba.

Mkurugenzi wa Shirika la Mawasiliano TTCL  Waziri Kindamba akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati wajumbe hao walipotembelea kituo cha Mawasiliano cha Mokongo wa Mawasiliano.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakijadiliana jambo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Bw. Waziri Kindamba akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Miundombinu wakati walipotembelea shirika hilo leo.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile katikati akiongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Suleiman Kakoso wa pili kutoka kushoto kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Jommy Yonaz na Mkurugenzi mkuu wa TTCL Waziri Kindamba.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile wa pili kutoka kulia akimsikiliza Mwenyelti wa kamati ya Kudumu ya bunge ya Miundombinu Mh. Suleiman Kakoso wakati akizungumza na wanahabari baada ya ziara hiyo  kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Waziri  Kindamba na kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo  Mbunge wa jimbo la Ikungi Mashariki Mh. Miraji Mtaturu.

Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo katika kituo cha Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa.

Leonard Laibu Meneja Biashara wa TTCL akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati hiyo wakati walipotembelea eneo maalum la makubusho ya vifaa vya mawasiliano vilivyotumika zamani

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imefurahishwa na utendaji kazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL katika juhudi ambazo wanazifanya hasa katika kusimamia mkongo wa Mawasiliano wa Kitaifa.

Akizungumza baada ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu kufanya ziara katika Shirika hilo leo mkoani  Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe.Selemani Kakoso amesema yapo mambo ambayo waliiagiza na yamefanyiwa kazi pia  wameridhishwa na namna utendaji kazi unaofanywa na TTCL.

“Serikali ilishafuta mikongo ya watu binafsi na kubaki na mkongo wa taifa ambao utasababisha ufanyaji kazi kwa usalama na ufanisi”. Amesema Mhe.Kakoso.

Aidha, Mhe.Kakoso amesema kwa taarifa ya Serikali imeweka makubaliano maalumu sasa TTCL atakuwa analipwa haki na stahiki zake kwa ajili ya kulinda mkongo wa taifa.

Hivyo basi Mhe.Kakoso amesema wamemuelekeza Mheshimiwa Waziri kusimamia taasisi za Serikali ambazo zinadaiwa na shirika la TTCL na POSTA watumiaji wengi hasa wa taasisi za serikali wamekuwa hawalipi gharama husika zile ambazo zinafanywa na mashirika hayo.

“Kwakuwa shirika haliwezi kuwadai, tumemuagiza Mheshimiwa Waziri alichukue waende wakaongee kama serikali kuhakikisha hizi taasisi ambazo zilitumia huduma za shirika la TTCL na POSTA waweze kulipwa Madeni”. Amesema Mhe.Kakoso.

Pamoja na hayo wameliomba shirika la TTCL wahakikishe sasa na wao wanajiendesha kibiashara kuliko kutegemea ruzuku kutoka serikalini .

“Tumewaagiza TTCL ili waweze kuimarisha vitengo vya mawasiliano vitakavyofanya sasa shughuli zao Iili waweze kujiendesha kibiashara”. Ameongeza Mhe.Kakoso.