Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Seleman Kakoso, akizungumza na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), Mhandisi Mahmoud Chamle, wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua miundombinu na vifaa vya kufundishia vya Taasisi hiyo, mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, mkoani Morogoro.
Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Rebeka Kimambo, akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, ukarabati wa majengo ya madarasa unaoendelea katika Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), mkoani Morogoro.
Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), Mhandisi Mahmoud Chamle, akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu maboresho na ukarabati unaoendelea wa Miundombinu ya Taasisi hiyo, mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipokagua Karakana ya Reli, mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiwa katika picha ya pamoja katika Karakana ya Reli iliyopo mkoani Morogoro.