Mkuu wa wilaya ya Bukoba moani Kagera aliye vaa miwani watatu kulia akikata utepe akiashiria kupokea na kuzindua adawati yaliyotolewa na shirika la World Vision kanda ya Kagera katika sherehe za maadhimisho ya miaka 40.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba moani Kagera aliye vaa miwani kushoto na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Bukoba na diwani wa Kata ya Rukoma Mhe. Murshidi Ngeze wakiwa wamekalia madawati waliyoyapokea kutoka shirika la World Vision kanda ya Kagera.
Wazazi, walezi na wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya kupokea madawati yaliyotolea na shirika la World Vision kanda ya Kagera, wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi wakati wa hafla hiyo, mkuu wa wilaya Bukoba Dedatus Kinawiro.
Wanafunzi wa shule ya msingi Ruzila wakipiga makofi wakiashiria kufurahia madawati waliyoletewa na shirika la World Vision ili kuwaondolea adha ya kukaa chini.
Wanafunzi wa shule ya msingi Ruzila wakibeba moja ya dawati
Muonekano wa baadhi ya madawati yaliyotolewa na shirika la World Vision kanda ya Kagera kwa shule za msingi za RUZILA, KABILIZI , BITUNTU na KAMKOLE zilizopo halmashauri ya wilaya Bukoba ili kurahisisha watoto kusoma vizuri.
……………………………………………………………………………………………….
Na Allawi Kaboyo – Bukoba.
Shirika la Warld Vision Tanzania Kanda ya Kagera Mach 04, mwaka huu, limeadhimisha miaka 40 tangu kuingia kwake hapa nchini kwa kutoa msaada wa madawati 350 kwa shule za msingi za RUZILA, KABILIZI , BITUNTU na KAMKOLE zilizopo halmashauri ya wilaya Bukoba ili kurahisisha watoto kusoma vizuri.
Akikabidhi Madawati hayo yenye thamani ya shilingi milioni 28 kaimu mratibu wa mradi wa Rukoma mbele ya mkuu wa wilaya ya Bukoba Mh. Deodatus Kinawiro, amesema kuwa mbali na shirika hilo kujitahidi katika kutoa huduma za kuisaidia jamii katika kujikwamua kiuchumi, wamekuwa wakitekeeza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Afya, Kilimo, Ufugaji, Maji pamoja na Elimu ili kumtengenezea mtoto mazingira rafiki ya maisha.
Ameonggeza kuwa shirika hilo linakabirina na changamoto za kuwepo kwa mimba za utotoni zinazo athiri malengo ya shirika yaliyolengwa ya kutaka kila mtoto apate elimu pamoja na jamii kuendelea kuwa tegemezi na kuwa na kipato kidogo hali inayopelekea kushindwa kumudu gharama za maisha ikiwemo Afya pia kuwepo kwa udumavu wa watoto wadogo chini ya umri wa miaka 5 pamoja na magonjwa mbalimbali.
Diwani wa Kata Rukoma ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mh. Murushid Ngeze amesema kuwa shule ya Msingi Ruzila imebadilika sana kutokana na ilivyokuwa hapo awali ambapo amesema kuwa kabla ya shirika la Word Vision kuwajengea vyumba vya madarasa na kuwaletea madawati walikuwa na vibanda vilivyotumika kama madarasa na chumba kimoja kilikuwa na mbao mbili za kufundishia.
Ngeze amesema kua wanafunzi walikuwa wanalazimika kusoma madarasa mawili ndani ya chumba kimoja wakikaa kwa kupeana migongo na masomo yanaendelea, ambapo ametumia fusa hiyo kulishukuru shirika hilo na kuliomba kuendelea kusaidia maeneo mengine yenye uhitaji.
Akipokea madawati hayo mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro amelishuru shirika la Word Vision Rukoma kwa ushirikiano mzuri na serikali katika kuhakikisha serikali inatimiza adhima yake ya kutoa elimu bila malipo na kuitaka jamiii kuendelea kujitoa na kulinda miundombinu wanayoletewa na serikali pamoja na wafadhili ili iweze kudumu na kuwasaidia watoto wao hapo badae.
Pamoja na hayo amewaonya wazazi wanaokataa kupeleka watoto wao shule wakati wamefikisha umri wa kwenda shule ambapo ameagiza watendaji wa vijiji na kata kuwachukulia hatua ifikapo mwisho wa mwezi wa 3/2021 huku akionya wale wote wenye tabia ya kuwarubuni watoto wadogo na kuwapa mimba na kukatisha ndoto zao sambamba na kuwaaharibia masomo yao kuwa waache tabia hio mara moja na wajue kufanya hivyo ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela.