Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akikabidhi kombe na Mbuzi kwa mwanafuzi wa kidato cha nne ambao ni washindi wa mchezo wa mpira wa miguu kwa wasichana katika kilele cha Mashindano ya Nyomi Cup yaliyoandalaliwa na Shule ya Sekondari Kihanga kwa wanafunzi wa shule hiyo iliyopo Wilaya ya Karagwe Mkoa Kagera, Machi 05, 2021
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akiongea wanafunzi, walimu pia wananchi waliojitokeza kwenye kilele cha Mashindano ya Nyomi Cup yaliyoandalaliwa na Shule ya Sekondari Kihanga kwa wanafunzi wa shule hiyo iliyopo Wilaya ya Karagwe Mkoa Kagera, Machi 05, 2021
Wanafuzi wa Shule ya Sekondari kihanga wakishangilia na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa baada ya kukabidhi makombe na zawadi mbalimbali kwa washindi Mashindano ya Nyomi Cup yaliyoandalaliwa na Shule ya Sekondari Kihanga kwa wanafunzi wa shule hiyo iliyopo Wilaya ya Karagwe Mkoa Kagera, Machi 05, 2021
……………………………………………………………………….
Na Eliud Rwechungura.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amepongeza shule ya sekondari Kihanga, Karagwe kwa kuanza utekelezaji kwa vitendo wa maelekezo ya kufundishwa kwa somo la michezo katika shule zote nchini yaliyotolewa Februali 08, 2021 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo.
Bashungwa ametoa pongezi hizo leo, Machi 05, 2021 kwenye kilele za Mashindano ya Nyomi Cup yaliyoandalaliwa na Shule ya Sekondari Kihanga kwa wanafunzi wa shule hiyo iliyopo Wilaya ya Karagwe Mkoa Kagera, yaliyohusisha Michezo ya Mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana, mpira wa pete, mpira wa wavu kwa wavulana na Wasichana, miruko ya juu na chini, mbio za umbali tofauti, kukimbia kwenye magunia na kukimbia na yai kwenye kijiko.
“Nipongeze Mkuu wa shule pamoja na Mwalimu wa michezo pamoja na walimu wote kwa kuanza kutekeleza maagizo yaliyotolewa na serikari kupitia Waziri Jafo, kwamba tunataka vipaji vya michezo tuanze kuviibua kuanzia shule za msingi na Sekondari, somo la michezo liwe somo muhumu kama yalivyo masomo mengine na hapa kihanga sekondari mmeonesha kwa vitendo utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kwahiyo mimi nawapongeza kwa kuwa shule mfano nchini”
Katika Kilele za mashindano hayo Waziri Bashungwa ametoa makombe na zawadi tofauti kama ifuatavyo; Kombe na mbuzi kwa washindi wa mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana, kombe na mbuzi kwa washindi wa mpira wa pete pia na zawadi ndogo ndogo kutokana na washindi michezo mingine.
Bashungwa amehaidi kuendelea kusaidia na kutoa ushirikiano wa kuhakikisha michezo inaendelezwa katika shule hiyo kwa kutoa mahitaji mbalimbali atakayopewa na mwalimu wa michezo ili shule ya sekondari kihanga iwe shule ya mfano kwa namna alivyokuta wanabuni wa kuendeleza michezo yote.
Naye, Mwalimu ya Michezo katika shule hiyo, Julius Jovinus amepongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha na kuwezeka mazingira wezeshi wa somo la michezo, pia akazitaja changamoto walizo nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa uwanja mzuri, ukosefu wa baadhi ya vifaa vya michezo kwa wanafunzi na Walimu pia upungufu wa vifaa vya utamaduni kama vile ngoma na vipuri.