Home Mchanganyiko RC NDIKILO AIAGIZA RUWASA PWANI KUSIMAMIA MIRADI ITEKELEZWE KWA WAKATI NA IWE...

RC NDIKILO AIAGIZA RUWASA PWANI KUSIMAMIA MIRADI ITEKELEZWE KWA WAKATI NA IWE YENYE UBORA

0
Na MWAMVUA MWINYI,PWANI
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ameuagiza wakala wa maji vijijini (RUWASA )Mkoa ,kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa miradi iliyopo kwenye mpango 2019-2021 kwa wakati na kuzingatia ubora na thamani ya fedha ili jamii inufaike na huduma ya maji.
Aidha ,amezitaka taasisi mbalimbali na wananchi kulipa ankara (bill) kwa wakati kwani baadhi ya taasisi na wateja wamekuwa wagumu kulipia na kusababisha miradi mingi kufa.
Alitoa agizo hilo ,wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya maji mkoa ,uliolenga kupokea taarifa ya utekelezaji 2019-2021 kutoka RUWASA na kusema ,kufikia Januari 2021 wastani wa wakazi asilimia 73 wanapata maji safi.
“Malengo hayo ni utekelezaji wa ilani ifikapo 2025 ,hivyo RUWASA kwa kushirikiana na jamii,viongozi na wadau mkoa kuongeza jitihada ilihali kufikia malengo ya kumfikia kila mwananchi aweze kupata maji safi.”
“Kwa vijijini wanapata maji kwa asilimia 71 na mijini ni asilimia 84 ” hatujafikia asilimia 11 kwa mijini na 14 vijijini ,ipo miradi haijakamilika na ipo katika utekelezaji ,RUWASA msimamie miradi hiyo iweze kuleta tija”alieleza Ndikilo.
Aidha Ndikilo aliitaka jamii kulinda na kutunza miundombinu ya miradi ya maji .
Awali meneja wa RUWASA Mkoani Pwani ,Beatrice Kasimbazi alieleza ,mkoa umepanga kutekeleza miradi 65 kwa gharama ya sh .bilioni 18.782.137.8 kwa kipindi cha mwaka 2021-2022 ambapo miradi mipya ni 17,upanuzi miradi 14 na ya ukarabati ni 34.
Kasimbazi alieleza kwamba,miradi inayoendelea kuanzia Julai 2019-februari 2021 ni miradi 48 ambayo inagharimu bilioni 9.829.086 na itanufaisha wakazi 99,334.
“Miradi mipy 16 gharama bilioni 8.403.232.5 na itanufaisha wakazi 77,760 pamoja na miradi 32 bilioni 1.425.853 kunufaisha wakazi 21,574.
Nae mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanal Patrick Sawala alieleza, malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wake Wilaya hiyo ni bili kubwa za maji kuliko uhalisia wa matumizi.
Kwa upande wa mwenyekiti wa halmashauri ya Mafia ,Juma Salum alisema wananchi wa Mafia wanalalamikia bili kubwa katika vituo vya maji ,wanaiomba mamlaka husika isimamie hilo .