Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akiwasili katika mitaa ya Mnyakongo, Bochela, Mtubi na Salama iliyopo katika kata ya Nkuhungu Jijini Dodoma mitaa ambayo imeathirika na mafuriko na kusababisha wakazi wa mitaa hiyo kukosa makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji leo March 4,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akizungumza mara baada ya kukagua mitaa ya Mnyakongo, Bochela, Mtubi na Salama iliyopo katika kata ya Nkuhungu Jijini Dodoma mitaa ambayo imeathirika na mafuriko na kusababisha wakazi wa mitaa hiyo kukosa makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji leo March 4,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akimsikiliza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru,wakati alipofanya ziara katika mitaa ya Mnyakongo, Bochela, Mtubi na Salama iliyopo katika kata ya Nkuhungu Jijini Dodoma mitaa ambayo imeathirika na mafuriko na kusababisha wakazi wa mitaa hiyo kukosa makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji leo March 4,2021 jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde ,akizungumza mara baada ya kukagua mitaa ya Mnyakongo, Bochela, Mtubi na Salama iliyopo katika kata ya Nkuhungu Jijini Dodoma mitaa ambayo imeathirika na mafuriko na kusababisha wakazi wa mitaa hiyo kukosa makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji leo March 4,2021 jijini Dodoma.
Muonekano wa nyumba zilizoathirika katika mitaa ya Mnyakongo, Bochela, Mtubi na Salama iliyopo katika kata ya Nkuhungu Jijini Dodoma mitaa ambayo imeathirika na mafuriko na kusababisha wakazi wa mitaa hiyo kukosa makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji leo March 4,2021 jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amefika katika mitaa ya Mnyakongo, Bochela, Mtubi na Salama iliyopo katika kata ya Nkuhungu Jijini Dodoma mitaa ambayo imeathirika na mafuriko na kusababisha wakazi wa mitaa hiyo kukosa makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji.
Akizungumza mara baada ya kufika katika mitaa hiyo na kujionea hali halisi Dkt Mahenge amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru kwa kushirikiana na timu ya wananchi na wataalamu wa jiji kufanya tathmini ya nyumba zote zilizozingirwa na maji na kuja na njia mbadala namna ya kuwasaidia wananchi hao ili serikali iweze kuona namna ya kuwasaidia.
“katika taarifa yenu mmeniambia kuna watu humu walipimiwa na iliyokuwa CDA na wengine wamevamia na kutokana na mvua zilizonyesha maji yamevuka eneo lake na kuingia kwenye makazi ya watu nataka mkurugenzi ufanye tathmini nyumba ngapi zimepata madhara na ni watu wangapi wanahitaji msaada.
“Pili kuna watu kwa jitihada za mbunge wamehifadhiwa na anawalipia kodi nataka nipate idadi na watu hao wanahitaji msaada kiasi gani, tunaweza kuongea na watu wa red cross tukapata matenti watu hawa wakawa salama” amesema Dkt Mahenge.
Ameongeza kuwa “Nashukuru nimefika nimejiridhisha katika nyumba zilizokatika maji hakuna watu wala sijapata taarifa ya maafa yoyote, hizi ni juhudi za mkuu wa Wilaya na Mbunge kuhakikisha wananchi wanakuwa salama kwa kuwapa elimu na baada ya tathmini kufanika nitakuja hapa junanne kufanya mkutano wa hadhara kutoa taarifa.
Amewataka wananchi kuondoka kabisa katika eneo hilo kwani ni hatari kwa Maisha yao na ametaka eneo hilo lisitumike tena hata kipindi maji yakipungua hata kama wana nyumba nzuri kiasi gani watu wasirudi tena katika hilo eneo badala yake watafutiwe maeneo mbadala yaliyokuwa salama kwa Maisha yao.
Amezitaka mamlaka husika kutengezeza kikosi kazi cha kuangalia namna ya kuondoa, kupunguza au kudhibiti maji hayo yasiweze kuendelea kuongezeka katika eneo hilo ili kuepusha madhara yanayoweza kutokana na watu kuishi karibu au kuzingirwa na maji.
Amesema jiji la Dodoma limezindua mpango kazi wa ardhi yote ya jiji la Dodoma wa mwaka 2019 hadi 2039 hivyo watu waepuke kununua maeneo bila kupitia mamalaka hiyo au kujenga nyumba bila kuwa na kibali kwani ni hatari unaweza jenga nyumba katika eneo ambalo sio eneo la makazi ikiwa na kuepuka kujenga maeneo ya milima.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru amemwambia mkuu wa Mkoa kuwa historia inaonyesha mwaka 1985 pembezoni mwa eneo hilo kulipimwa viwanja na eneo dogo likabaki kuwa eneo la maji lakini baadhi ya watu wakaingia na kujenga pembezoni na miaka miwili ya karibuni kutokana na mvua kubwa zilizonyesha maji yamevuka na kuingia katika makazi ya watu.
Amesema mara kadhaa wamejaribu kuondoa maji hayo lakini tathmini inaonyesha ikiondoa maji hayo yanakwenda kuleta athari katika maeneo mengine yaliyosalama hivyo wapokatika mchakato wa kufanya tathmini ya idadi ya watu ili watafutiwe eneo salama kwa makazi.
Nae Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mhe. Antony Mavunde ameshukuru kwa Mkuu wa Mkoa kuagiza kufanyika kwa tahmini hiyo na ameomba ifanyike haraka ili wananchi hao waweze kupata makazi mbadala kwani baadhi ya wenye nyumba maeneo hayo wamepandisha kodi za nyumba kwa sababu wengi hawana makazi na wananchi wengi hawana uwezo wa kulipa kodi kwa miezi sita.