Kushoto ni Kocha wa timu ya AFC Elly Kisanga, Katikati ni mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt John Pima na kulia ni Afisa michezo wa jiji la Arusha Benson Maneno
……………………………………………………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt John Pima amekabidhi mipira mitano kwa timu ya mpira wa miguu Arusha {AFC} baada ya kusikia changamoto ya timu hiyo katika vyombo vya habari na kuifuatilia.
Akikabidhi mipira hiyo Dkt Pima kwa kocha wa timu hiyo alisema kuwa jiji hilo ni wadau wa michezo kwahiyo wameona wamesikia na kuona changamoto ya mpira na kuona kuwa wanawajibu wa kuwasidia kwani ni timu inayotoka ndani ya jiji.
“ Sisi viongozi wa serikali na wabunge na madiwani wote tunapenda michezo ndio mana tumeona tuwape mipira hii kama hatua za mwanzo za kuwasaidia ili kuwawezesha kufanya michezo hii vizuri ili kila mnapokwenda mkaiwakilishe vema jiji la Arusha,” Alisema Dkt Pima.
Alieleza kuwa huo ni mwendelezo wa juhudi za rais John Magufuli za kuhakikisha kserikali haijitengi na michezo kwani anapenda michezo na anataka kama taifa wajiandae vizuri wanapokwenda kushindana popote ndani na nje ya nchi.
“Huu ni mwendelezo wa juhudi kubwa anazofanya Muheshimiwa Rais kwamba serikali haijitengi na wanamichezo bali inakuwa bega kwa bega kwa kuhakikisha inaboresha na kufanya mabadiliko makubwa katika kukuza na kuinua michezo nchini,” Alieleza.
Alifafanua kuw watakuwa wana wasapoti lakini pia ataagiza idara ya michezo kuwa karibu na timu hiyoili waweze kuisaidia timu kutoka ligi daraja la pili na kuingia ligi kuu kwani michezo ni ajira na inachangia pato la taifa ambapo pia wana mikakati ya kutafuta timu ya kuisapoti na kuifanya iwe timu ya jiji rasmi.
Kwa upande wake kocha wa timu ya AFC Elly Kisanga alisema kuwa kwa niaba ya wachezaji, wanachama na viongozi wanaahidi kuwa kutokana na mipira hiyo wataenda kufanya vizuri zaidi kwani awali walikuwa na mipira miwili peke yake.
Aidha alisema kuwa bado wana changamoto ya viatu lakini pia chakula hivyo mdau yoyote atayeona anaweza kusauidia anakaribishwa .