Home Mchanganyiko MKAZI WA KIJIJI CHA MPENDOO NCHEMBA ANASWA NA DAWA ZA SERIKALI

MKAZI WA KIJIJI CHA MPENDOO NCHEMBA ANASWA NA DAWA ZA SERIKALI

0

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Kanda ya Kati mnamo tarehe 2.03.2021 ilifanya ukaguzi katika maeneo yanayojishughulisha na biashara ya dawa na vifaa tiba katika kijiji kiitwacho Mpendoo kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba. Ukaguzi huo ulifanikisha kukamata dawa za Serikali aina saba (7) zenye thamani ya Tsh. 265,000/= katika duka la dawa muhimu liitwalo ROGECHU. Mtuhumiwa amekamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Chemba ambapo anashikiliwa na Jeshi la Polisi. Taratibu nyingine za kumfikisha mtuhumiwa mahakamani zinaendelea.