WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Magari kwa ajili ya Utoaji Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Magari kwa ajili ya Utoaji Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu,TAMISEMI, Gerald Mweli,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Magari kwa ajili ya Utoaji Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, TAMISEMI, Dk.Ntuli Kapologwe,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Magari kwa ajili ya Utoaji Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la IntraHealth International, Dk. Lucy Mphuru, akieleze jinsi shirika hilo linavyotoa huduma za kijamii hapa nchini wakati wa uzinduzi wa Magari kwa ajili ya Utoaji Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
Muwakilishi wa waganga wakuu wa Mikoa ya Mwanza,Shinyanga,Simiyu na Mara ambaye pia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Shinyanga Dk.Nuru Mpuya akitoa neno la shukrani kwa niaba mara wakati wa uzinduzi wa Magari kwa ajili ya Utoaji Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki pamoja na Waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Magari kwa ajili ya Utoaji Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
Haya ndio Magari Matatu yaliyotolewa kwa mikoa Mitatu kwa ajili ya utoaji wa Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume hafla iliyofanyika leo March 4,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Magari kwa ajili ya Utoaji Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,akieleza jambo mara baada ya kuingia ndani ya Gari na kujionea huduma bora za Utoaji Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,akimsikikiliza Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, TAMISEMI, Dk.Ntuli Kapologwe, ndani ya gari la kutoa Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la IntraHealth International, Dk. Lucy Mphuru,wakiwa ndani gari la kutoa Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,akionyeshwa juu na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Afya Plus Dk.Pastory Sekule mara baada ya kuzindua Magari kwa ajili ya Utoaji Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua wa Magari kwa ajili ya Utoaji Huduma Tembezi za Tohara kwa Wanaume Kanda ya ziwa hafla iliyofanyika leo March 4,2021 katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………….
Na Alex Sonna, Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo, leo amezindua huduma ya afya tembezi kwa ajili ya tohara kinga kwa wanaume kwenye mikoa minne ya Kanda ya Ziwa.
Mikoa hiyo ni Mwanza, Simiyu, Mara na Shinyanga.
Huduma hiyo itatolewa kwenye magari maalum ya kisasa ambayo yamegharimu Sh.Bilioni 1.2 ambayo yametolewa na Shirika la Intra Health International kwa ufadhili Mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi(PEPFAR) kupitia Kituo cha Kimataifa cha kujikinga na maradhi(CDC).
Akizindua huduma hiyo leo March 4,2021 jijini Dodoma Waziri Jafo amewataka wanaume ambao hawajatahiriwa kuchangamkia huduma hiyo kwenye maeneo yatakayopangwa kwa kuwa tafiti zimeonyesha tohara inamkinga mwanaume kutopata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) kwa zaidi ya asilimia 60.
Amesema huduma ya tohara zilikuwa zinatolewa katika vituo vya kiutolea huduma za afya kwenye mikoa 19 ambayo ina maambukizi makubwa ya VVU na uwiano mdogo wa wanaume waliopatiwa huduma ya tohara.
“Aidha, ili kuweza kuwafikia wanaume wengi wenye mahitaji ya kufanyiwa tohara na pia wanaoishi sehemu ambazo ni ngumu kufikika, serikali kwa kushirikiana nan a wadau imeamua kununua magari matatu kwa ajili ya kutoa huduma tembezi,”amesema.
Ameagiza kuhakikisha magari hayo yanatunzwa kwa ufasaha ili yatoe huduma kwa muda mrefu huku akiwashukuru wadau hao kwa kuendelea kushirikiana na serikali kwenye kuboresha utoaji wa huduma za afya ya msingi.
Awali, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la IntraHealth International, Dk. Lucy Mphuru, amesema wanaume Milioni 1.82 wa mikoa hiyo minne wamepata huduma ya tohara huku watumishi 1,000 wa afya wakipatiwa mafunzo ya utoaji huduma bora za tohara tangu mwaka 2010 hadi sasa.
Amesema magari hayo ni ya kisasa na ni ya aina yake hapa nchini ambapo yana vi8faa vyote muhimu vya kutolea huduma ya tohara pamoja na huduma zingine za afya.
“Shirika la IntraHealth litaendelea kuunga mkono na kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi kulingana na sera, taratibu na miongozo ya serikali,”amesema.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu,TAMISEMI, Gerald Mweli amesema serikali imekeza kwa kiwango kikubwa kwenye kuboresha huduma za afya, ununuzi wa vifaa tiba na kuajiri watumishi.
Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, TAMISEMI, Dk.Ntuli Kapologwe, amesema serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma vinavyogharimu Sh.Bilioni 68 kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma ya tohara.