Mhandisi Gasto Mkawe akimweleazea mkuu wa wilaya ya Arusha na madiwani wa halmashauri ya Jiji la Arusha utekelezaji wa mradi wa maji wa billion 520 ulipofikia.
Madiwani wa Jiji la Arusha na mkuu wa wilaya Arusha wakiangalia kituo cha kutibu Maji cha Midawe.
Bwawa la maji taka lililopo katika Kata ya Terrat jijini Arusha.
Mhandisi Gasto Mkawe Mratibu wa miradi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira( AUWSA) Akionyesha ramani ya jinsi mradi wa Maji wa billion 520 utakavyokuwa.
Diwani wa kata ya Sekei Gerald Sebastian akiongea katika ziara ya kukagua mradi wa Maji wa billion 520.
…………………………………………………………………….
NANAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Madiwani wa wa halmashauri ya jiji la Arusha wameahidi kwenda kuwaeleza wananchi mafanikio makubwa yatakayo patikana baada ya mradi wa maji wa billion 520 kukamilika moja wapo ikiwa ni kumalizika kwa changamoto ya maji kwa zaidi ya miaka 25 ijayo.
Madiwani hao waliyasema hayo baada ya kutembelea mradi huo unaendelea kutekelezwa kufuatia ziara iliyoandaliwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi amabpo waliweza kutembelea upande wa maji safi na maji taka.
Gerald John Sebastian Diwani wa kata ya Sekei alisema kuwa katika kata yake upande wa mita mia mbili bado kuna changamoto kubwa ya maji ambapo bado akina mama wengi wanabeba maji kichwani hivyo ni matarajio yake baada ya mradi kukamilika utasaidia kutatua tatizo hilo.
Sebastian alieleza kuwa shida za maji ambazo anapigiwa kelele na wananchi wake baada ya kuutembelea mradi huo na kusikiliza jinsi utakavyo wahudumia wananchi anaamini tatizo la maji liitaisha kabisa katika kata yake.
“Kwa makusidio haya kama wanavyosema mradi huu utaisha Octoba 2021 na mimi kama mheshimiwa diwani nitapata faraja kwasababu akina mama wengi kila kukicha wanapiga kelele wakilalamikia changamoto ya maji itakuwa ndo mwisho wa malalamiko yako na wataendelea kuiamini na kuitumikia serikali yao kwa furaha,” Alisema Sebastian.
Aidha alisema kuwa pia kuna changamoto ya bili za maji kuwa kubwa na watu wengi kwenye kata yake wamekuwa wakililalamikia hilo ambapo kuna baadhi ya watu walikuwa wakilipa shilingi elfu 3000 hadi elfu 5000 sasa hivi wanalipa zaidi hata ya elfu 30000 jambo ambalo sio sawa lakini kupitia ziara hiyo wameweza kupata majibu kuwa mamlaka ya na usafi wa mazingira{Auwsa} wanalifuatilia jambo hilo ili kuondoa changamoto hiyo inayolalamikiwa na wananchi katika maeneo mengi.
Diwani wa kata ya Engutoto Karim Moshi alisema kuwa kwnye ilani ya chama cha mapinduzi kuna agenda ya kumtua mama ndoo kichwani ambapo kupitia mradi huu imetekelezwa kwa vitendo ambapo hata watu wanapozidi kuja Arusha na jiji kuendelea kupanuka maji safi ya kutosha yapo lakini pia eneo la kuhifadhi maji taka lipo.
“Changamoto ilikuwa ni kubwa sana kuna watu wapo hapa mjini kwa zaidi ya miaka 20 lakini hadi leo wanabeba maji kwa kutumia kichwa lakini tangu mradi huu uanze mabomba yanapasuka kutokana na wingi wa maji hivyo wanaishukuru serikali kwani imeweza kutambua shida za wananchi na kuweza kuzitatua,” Alisema Moshi.
Diwani wa Kata ya diwani wa kata ya Elerai Losioki Moikan Laizer ameishukuru serikali ya Rais Maghufuli kwani mradi huo ni mkubwa na unaonesha kuondoa changamoto ya maji kabisa ambapo watarudi kwa wananchi wao na kwenda kuisemea serikali yao vizuri juu ya mradi huo utakavyosaidi na hiyo inadhiirisha kuwa wamekomaa sasa kuelekea uchumi wa kati ulioimarika.
Kwa upande mkuu wa wila ya Arusha Kenan Kihongosi alisema kuwa maji yamekuwa ni kilio kila eneo na madiwani wamekuwa wakimpigia simu kutaka kujua ni lini changamoto hiyo itabata majibu kutokana na wananchi kuwauliza kila siku ambapo lengo la ziara hiyo ni madiwani kwenda kuona mradi huo, kujua utafanyaje kazi lakini pia kujua ni lini utakamilika ili waweze kupata maji ya kuwajibu wananchi ambao ndio wanaowawakilisha.
“Baada ya kuutembelea mradi huu ninaamini mmepata majawabu ya kutosha ambayo yatawasaidia kwenda kuwaelimisha wananchi kwani kinachofanyika ni utekelezaji wa ilani ya chama mapinduzi ambayo sisi ndio tunaosimamia utekelezaji wake kwa hiyo mkirudi kwa wananchi wenu mkawaambie nini Dkt Magufuli amewafanyi ,” Alieleza Kenan.
Naye mratibu wa mradi kutoka mamlaka ya maji na usafi wa mazingira{AUWSA} Injinia Gasto Mkawe akielezea mradi huo alisema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 94 ambapo visima 30 vimeshachimbwa na saba tayari vinafanya kazi na unatarajiwa kuongezeka kwa mtandao wa mabomba ya maji kwa kilometa elfu 900 ambapo utawaunga watu zaidi ya elfu 4500 huku elfu 2000 wakiwa tayari wameshaunganishiwa.
Eng; Mkawe alisema kuwa upatikana naji wa maji awali ulikuwa ni million 40 kwa siku huku mahitaji yakiwa ni million 106 kwa siku ambapo mradi huo ukikamilika uzalishaji utakuwa ni million 45 kwa mara moja na usanifu wa mradi huo umelenga kuondoa changamoto ya maji kwa miaka 20 hadi 25 ya mbele na umekizi mahitaji ya ongezeko la maji.
Aidha akielezea bwawa la maji taka la kisasa linaloendelea na utekelezaji latika kata ya Terrat Injinia Mkawe alisema kuwa wamejenga mabwawa 18 ya kisasa ambayo yatapokea maji taka kutoka mjini na kuingia katika hatua ya kutaibu na baadaye kuweza kurudi katika mzunguko wa maji kwenye mito ambapo yatafaa kwaajili ya umwagiliaji.
“Mabwawa haya yanauwezo wa kutibu maji lita million 22 kwa siku ambapo kwasasa yanaingia lita million 6.5 kwa siku kutoka kwa wateja 1200 ambao wameshaunganishwa moja kwa moja na kutoka katika mabwawa ya zamani yaliyopo katika kata ya Lemara ambapo tunaendelea kuwaunganisha wateja wengine wapya,” alisema.