Ni mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya Diamond Gin akielezea bidhaa za pombe wanazozizalisha
*************************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Kampuni ya Diamond inayojishugulisha na utengenezaji wa pombe zenye ladha tatu tofauti wanatarajia kufungua tawi mkoa wa mwanza ili kuweza kuwafikia watanzania wengi zaidi.
Hayo yalisemwa na meneja mauzo na masoko wa Kampuni hiyo Mustapher Pirbhai wakati akielezea bidhaa za vinywaji wanazozalisha katika fainali za Bonanza la Arusha super cup ambapo alisema kuwa pamoja na kuwa Kampuni hiyo makao makuu yake ni Arusha, wameenea maeneo mbalimbali ya nchi lakini pia wanatarajia kufika mwanza hivi karibuni.
Mustapher alisema kuwa wanazalisha vileo vyenye ladha tatu ambavyo ni yenye ladha ya Nanasi, strawberry pamoja na Gin halisi ambayo haina harufu wala uchovu huku wakiwa na wafanyakazi zaidi ya 40.
“Pombe yetu ina kilevi 37.5, Ni nzuri sana hivyo nawahamasisha watanzania kuendelea kunywa kinywaji cha Diamonds Gin ambacho hakina harufu wala uchovu(hangover) ambazo itawafanya wasijutie kutokana na uzuri wake,” Alieleza Mustapher.
Aidha akizungumzia Bonanza hilo lenye alisema kuwa ni jambo zuri Wana Arusha wamekutanishwa ili kuweza kukuza michezo lakini pia kuimarisha afya zao kupitia michezo mbalimbali inayoendelea.
“Bonanza hili kimefanikiwa kwa asilimia kubwa kwani watu ni wengi japo kuna changamoto ya michezo mingi kuchezwa kwa wakati mmoja kwa mfano huku unakuta mpira wa miguu na upande ule mpira wa pete sasa mashabiki tunatamani tuone yote nafikiri wakati mwingine siku za fainali ziongezwe ili tuweze kufaidi michezo yote,” Alieleza.