Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme TANESCO. Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka akiwakaribisha Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali katika semina ya shirika hilo inayofanyika kwenye ukumbi wa NSSSF mjini Morogoro leo toa ufafanuzi wa baadhi ya hoja ambapo pia ametoa ufafanuzi wa hoja kadhaa zilizotolewa na wahariri katika semina hiyo.
………………………………….
Shirika la umeme nchini (TANESCO),limesema hali halisi ya umeme katika mabwawa yote saba ya kuzalisha umeme kwa njia ya maji nchini, iko vizuri na kwamba wanatarajia hivi karibuni kuyafungilia maji katika bwawa la mtera,kufutia maji kufikia kiwango stahiki ili kulilinda bwawa.
Mhandisi Steven Manda,ambaye ni Meneja mwandamizi wa Ufuaji Umeme kutoka TANESCO,amesema hayo wakati akiwasilisha mada ya hali halisi ya uzalishaji umeme nchini,wakati wa kikao kazi cha siku 3 cha TANESSCO na Wahariri waandamizi wa Vyombo mbalimbali vya habari nchini,kinachofanyika kwenye ukumbi wa NSSSF Mkoani Morogoro.
Mhandisi Manda,amesema,kwa sasa bwawa la Mtera,limevuka uwezo wake wa mita za ujazo 698.76 na kwamba ni hatari kwa usalama wa miundombinu yake kama wataacha maji yaendelee kuwepo kwa kiwango kilichozidi.
Katika hatua nyingine, (TANESCO),imesema,maji yanayofunguliwa hayatupwi iasipokuwa yanatumika kwa matumizi mengine ya binadamu ikiwemo kweye mabonde mbalimbali ya kilimo cha umwagiliaji, kunywesha mifugo N.k.
Akisisitiza zaidi Mkutrugenzi Mtendaji wa Shirika la Umete TANESCO Dk. Tito Mwinuka amesema hata huo uwezo wa kuhifadhi maji wakati mwingine unazidi.
Kwa mfano sasa Mtera likijaa mkafungulia na Kihansi likajaa Mkafungulia kama Bwawa la Nyerere likikamilika maana yake mkifungulia maji yatakwenda moja kwa moja kwenye Bwawa la Nyerere ambalo ni kubwa na lina uwezo wa kuhifadhi maji kwa wingi hivyo Bwawa hilo litakuwa na faida nyingine kubwa ya kuhifadhi maji ya kutosha wakati mabwawa mengine yanapokuwa yamejaa maji.
Meneja Mwandamizi wa Uzalishaji Umeme (Power Generation) kutoka Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Mhandisi Stephen Manda akiwasilisha mada katika semina ya wahariri wa vyombo vya habari inayofanyika kwenye ukumbi wa NSSSF mjini Morogoro.
Meneja Uhusiano TANESCO Bi. Johary Kachwamba akiwasilisha ratiba ya mkutano ukiendelea kabla ya kuanza rasmi.
Liliano Timbuka Mhariri kutoka Gazeti la Mwananchi na Freddy Mwanjala Ofisa kutoka Idara ya Habari Malelezo Dodoma wakifuatilia mada katika semna hiyo.
Mhariri wa ITV Steven Chuwa aliyeketi mbele pamoja na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Majira Emmanuel Mbuguni na Scolastica Mazula wakifutilia mada katika semina hiyo.
Baadhi ya watoa mada kutoka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO na taasisi zake wakiwa katika semina hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Umeme TANESCO Grace Kisyombe kulia akiwa pamoja na Francis Maze wakiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa Uhusuano Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Johari Kachwamba kulia akiteta jambo na Ofisa Uhusiano wa Shirika hilo B. Samia Chande.
Kutoka kulia ni Ekland Mwafisi Mhariri wa Gazeti la Lajiji, Mgaya Kingoba kutoka Gazeti la Habari Leo na Steven Chuwa katikati.
Mhariri wa Clouds Media Bi. Joyce Shebe ni miongozi mwa wahariri wanaohudhuria katika semina hiyo.
Meneja Mwandamizi wa Uzalishaji Umeme (Power Generation) kutoka Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Mhandisi Stephen Manda akifafanua baadhi ya hoja zilizotolewa na wahariri wa vyombo vya habari katika seminahiyo.