*******************************
NA EMMANUEL MBATILO, MTWARA
Ujenzi wa miundombinu iliyotekelezwa na Serikali imeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa Uchumi wa nchi ikifuatiwa na kilimo pamoja na ukuaji wa viwanda katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015 hadi 2019.
Akizungumza katika semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari za Uchumi na fedha yaliyofanyika katika Tawi la Benki Kuu ya Tanzania Mkoani Mtwara Mchumi wa BoT Bw.Aristides Mrema akiwasilisha Mada alisema kuwa japokuwa kuwepo kwa changamoto ya Covid -19 inayoikumbwa Dunia kwa ujumla, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizokuwa kiuchumi.
“Ukiangalia sekta ambazo zimeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji huu wa uchumi ni ujenzi asilimia 25,kilimo (20) viwanda (9.6),usafirishaji na uhifadhi mizigo (8.3) na biashara 7.3”. Alisema Bw.Mrema .
Aidha Bw.Mrema alisema kuwa takwimu za Januari hadi Septemba mwaka jana zinaonesha pato la taifa kukua kwa asilimia 4.7 ukilinganisha na asilimia 7.9 mwaka 2019 na asilimia 6.9 mwaka 2018.