Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Nne na Tano katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora wakiimba wimbo wa uzalendo wa Tanzania , Tanzania Nakupenda wakati hafla fupi jana ya kupokea msaada wa fedha kiasi cha shilingi milioni 9.9 kutoka MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji(EWURA) kwa ajili utengenezaji wa dawati.
Meneja wa Kanda ya Kati wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji(EWURA), Meneja wa Kanda ya Kati, Mhandisi Norbert Kahyoza (kushoto) akimkabidhi jana Katibu Tawala wa Wilaya ya Tabora Yonaza Hammarskjod(kulia) kwa niaba ya Shule ya Wasichana ya Tabora.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Tabora Yonaza Hammarskjod akitoa maelezo mafupi jana baada ya kupokea hundi ya shilingi milioni 9.9 ikiwa mcha wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) wa kutengeneza dawati katika Shule ya Wasichana ya Tabora .
Meneja wa Kanda ya Kati wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji(EWURA), Norbert Kahyoza akitoa maelezo mafupi jana baada ya kukabidhi shilingi 9.9 kwa Shule ya Wasichana ya Tabora ili ziwasaidie katika utengezaji wa dawati 247.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora Lydia Eliud akitoa maneno ya shukurani jana baadaya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji(EWURA) kukabidhi shilingi 9.9 kwa Shule hiyo ili ziwasaidie katika utengezaji wa dawati 247.
Baadhi walimu wa shule ya sekondari ya wasicahana Tabora wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Kudhibiti Nishati na Maji(EWURA) jana baada ya kukabidhi shilingi 9.9 kwa Shule ya Wasichana ya Tabora ili ziwasaidie katika utengezaji wa dawati 247.
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
24 Feb. 21
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji(EWURA) imetoa kiasi cha shilingi milioni 9.9 kwa ajili ya utengenezaji wa madawati 247 katika Shule ya wasichana ya Tabora(Tabora Girls).
Fedha hizo zimekabidhiwa jana na Meneja wa Kanda ya Kati, Mhandisi Norbert Kahyoza kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tabora Yonaza Hammarskjod kwa niaba ya Shule ya Wasichana ya Tabora.
Alisema sehemu kubwa ya shughuli za EWURA zinaambatana na masuala ya sayansi na ndio maana wakaamua kuunga mkono Shule ya Sekondari ya wasicha Tabora kwa kutambua wapo wanafunzi wengi wanasomo masomo ya sayansi.
Mhandisi Kahyoza alisema hatua hiyo inalenga kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na kuwa mazingira ya kujifunzia na kusoma.
Aidha Meneja huyo wa Kanda aliutaka uongozi wa Shule ya Wasichana kuhakikisha wanaharakisha kutengeneza madawati ili fedha hizo zisije zikatumika kwa shughuli nyingine pindi ikitokea dharura.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Halima Sangali alisema fedha walizopatia Shule ya Wasichana ya Tabora zitawasidia kupunguza upungufu wa dawati 349 hadi kubaki na upungufu wa dawati 102.
Alisema watatengeneza dawati 247 kwa gharama ya kila mmoja shilingi 40,000/= na kuongeza kuwa watajitahidi kufanyakazi haraka ili wanafunzi waanze kunufaika na mchango wa EWURA.
Kwa upande wa Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana Tabora ambaye pia ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano masomo ya Fikizia, Kemia na Baolojia (PCB) Nice Timanywa aliishukuru EWURA kwa msaada huo ambao umewasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa dawati.
Alisema upungufu wa dawati ulisababisha baadhi ya wanafunzi kupata matatizo ya mgongo na wengine kushindwa kufanya vizuri kutokana na mazingira ya ukaaji darasani.
Nice alisema msaada waliopata ni deni kubwa kwao ambalo wanapaswa kulilipa kwa kuongeza ufaulu ili EWURA watakaoona matokeo waone hajakosea kuwasaidia.