Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza katika kikao kazi kilichoandaliwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo ambacho kimewajumuisha walimu wakuu wa shule za sekondari za serikali kutoka Wilaya zote kwa lengo la kuweza kujadili na kupanga namna ya kuweza kuboresha sekya ya elimu na kukuza kiwango cha ufaulu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere akizungumza na walimu wakuu wapatao 85 hawapo pichani kutoka shule mbali mbali za sekondari ambazo zinamilikiwa na serikali ili kujadili namna bora ya kukuza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi na kujadili mikakati ya kuboresha elimu kwa ujumla.
………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, PWANI
MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amechukizwa na baadhi ya walimu ambao ni wazembe katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika kuwafundisha wanafunzi na kuwagiza wakuu wote wa shule za sekondari kubadilika na kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti ambayo itaweza kuongeza kasi ya ufundishaji ili kuboresha sekta ya elimu na kusaidia kasi ya kiwango cha ufaulu iweze kuongezeka hasa katika shule za serikali.
Ndikilo ametoa kauli hiyo wakati wa kufungua kikao kazi ambacho kimewakutanisha wakuu wa shule za sekondari za serikali wapatao 85 kutoka Wilaza zote za Mkoa wa Pwani kwa lengo la kujadili mikakati madhubuti ambayo itasaidia kuinua kiwango cha elimu kwa wanafunzi na kuwataka wakuu wote wa shule kulivalia njuga suala hilo na kuwachukulia hatua kali walimu amabo ni wazembe.
Aliongeza kwamba lengo la serikali ya Mkoa wa Pwani ni kuhakikisha kwamba inaweka mipango madhubuti kwa ajili ya kuongeza kasi zaidi kwa wanafunzi wetu wa wanaosoma katika shule mbali mbali za serikali hivyo walimu wote mnapaswa kuongeza juhudi zaidi katika kutilia mkazo suala zima la kuwafundisha wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
“Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani uwa nashangaa sana kuona katika shule zingine zinafanya vizuri na zingine zinafanya vibaya kwa hivyo rai yangu na maagizo kwa wakuu wote wa shule za sekondari amabzo ni zaserikali lazima sasa mhakikishe mnawafuatilia kwa ukaribu walimu wote ambao ni wazembe katika ufundishaji maana haiwezekani mwalimu anapokea mshahara lakini katika kuwafundisha wanafunzi hafanyi hivyo hii sio sahihi hata kidogo,”alisema Ndikilo.
Aidha Ndaikilo aliongeza kuwa ili wanafunzi wa shule za serikali waweze kufanya vizuri katika mitihani yao mbali mbali ya Taifa inatakiwa kuwe na ushirikiano wa karibu baina na walimu wakuu pamoja na walimu wa kawaida katika suala zima la kuweza kuwaandaa mapema wanafunzi ili wanapoingia katika mitihani yao wanakuwa wameshajiweka katika maandalizi mazuri.
Katika hatua nyingine Ndikilo aliwapongeza wallimu wakuu hao wa shule za sekondari za serikali kwa kuweza kujitahidi kwa ahali na mali kuongeza kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka na kuwataka waendelee na moyo huo huo wa kuongeza juhudi na mahalifa zaidi ili Mkoa wa Pwani uweze kuingia katika tano bora katika ngazi ya Taifa.
Kwa upande wale Afisa elimu wa Mkoa wa Pwani Khadija Mcheka amesema kwamba licha ya kiwango cha elimu elimu ya sekondari kuongezeka kwa asilimia 85.8 ukilinganisha na miaka iliyopita lakini bado kuna changamoto zilizopo katika sekta hiyo ikiwemo ya miundombinu ya majengo ya madarasa, pamoja na uhaba wa vitendea kazi ambavyo vinahitajika ili kuboresha sekta ya elimu.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere amabye ndie aliyeitisha kikao kazi hicho alibainisha kwamba dhumuni kubwa ni kuwakutanisha wakuu wote wa shule hizo za sekondari serikali ni kwa lengo la kuweza kujadili changamoto zilizopo katika sekta ya elimu ili kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mbinu zitakazosaidia kuongeza kiwango cha elimu.
Pia Dk. Magere aliongeza kuwa ana imani kikao kazi hicho katia ya walimu wakuu kitaweza kuleta chachu zaidi ya kukuza kasi ya maendeleo katika sekta ya elimu na kwamba katika siku zijazo wanatarajia wanafunzi wanaosoma katika shule mbali mbali za serikali wataweza kufanya vizuri zaidi tofauti na miaka iliyopita.
“Hiki kikao nimekiandaa kwa lengo la kukutana na walimu wakuu wa shule mmbali mbali za serikjali na hapa wamekuja walimu wapatao 85 kwa hivyo ni imani yangu tutaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea ya Mkoa wetu wa Pwani kuingia katika nafasi ya tano bora kitaifa na ili siis tunaliweza endapo tukishikamana kwa kwa sasa utaona ufaulun wetu kwa shule za sekondari umeongezea hadi kufikia alimia 85 na tutaendelea na kasi hii.”alisema Dk. Magere.
SERIKALI Mkoani Pwani kupitia kwa Katibu Tawala wake Dk. Delphine Magere imeamua kuwakutanisha kwa pamoja walimu wakuu whao 85 kutoka shule mbali mbali za serikali za Mkoa kwa lengo la kuweza kuweza kujadili changamoto mbali ,bali ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi lengo ikiwa ni kuongeza kasi zaidi ya ufaulu kwa wanafunzi.