Home Mchanganyiko SIMBACHAWENE AIAGIZA NIDA KUMALIZA UZALISHAJI WA VITAMBULISHO VYA WANANCHI WENYE NAMBA MIL.12...

SIMBACHAWENE AIAGIZA NIDA KUMALIZA UZALISHAJI WA VITAMBULISHO VYA WANANCHI WENYE NAMBA MIL.12 NCHINI

0
………………………………………………………………………………
Na MWAMVUA MWINYI,PWANI
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ,George Simbachawene ameiagiza , mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA)kuhakikisha wanamaliza kilio cha wananchi waliotambuliwa na kukosa vitambulisho wapatao milioni 12 nchini,”, kwa kuhakikisha wanazalisha vitambulisho hivyo ifikapo July mwaka huu .
Aidha ameielekeza NIDA kushirikiana na taasisi nyingine za kiserikali waweze kuweka matumizi yote ili kufanyika shughuli nyingine za kiuchumi badala ya utambulisho wa utaifa pekee.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Pwani ,baada ya kutoka kutembelea na kukagua mitambo mipya kwenye jengo la NIDA lililopo Kibaha Mjini,alieleza, uwezo wa NIDA kuzalisha Vitambulisho kwa kizazi cha kwanza ni vitambulisho 1,000 -1,200 kwa saa ambapo kwa masaa 16 inatoa vitambulisho 32,000 -35,000 ili kumaliza kadi za zamani milioni tano (5).
“Baada ya hapo wataanza kwa kizazi cha pili kwa kutoa vitambulisho 4,000-4,500 kwa lisaa limoja na masaa 16 itakuwa na uwezo wa kutoa vitambulisho 72,000 -75,000 mbapo kwa siku moja watakuwa kama wanamaliza wilaya moja .” alifafanua .
Alieleza ,mkakati wa NIDA ni kumaliza vitambulisho hivyo mwezi agost mwaka huu lakini kutokana na kuna na mfumo wenye kasi zaidi ambao unaondoa ucheleweshaji hakuna sababu ya kuchelewesha .
“Ongezeni kasi ya uzalishaji ,kwani kuna wenye namba hadi Leo lakini hawana vitambulisho” alifafanua Simbachawene.
Simbachawene alisema ,changamoto ya zamani ilikuwa uchakavu wa mitambo ya zamani na serikali ikaliona hilo na kuleta mitambo mipya.
Waziri huyo aliwataka pia ,kuangalia namna ya kugawa vitambulisho wanavyomaliza kuzalisha kwa wilaya zote badala ya wilaya moja moja hali inayosababisha kuchelewa kutoa huduma kwa walengwa.