Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini( TANESCO) mkoani Manyara, wakati wa mkutano wake na wafanyakazi hao wenye wenye lengo la kufahamiana, kusikiliza changamoto zinazowakabili pamoja na kutoa maelekezo ya kuboresha utendaji kazi wa shirika hilo uliofanyika Februari 17, 2021 mkoani humo.
,……..,….,,..,…,,..,.,,
Na Zuena Msuya, Manyara
Naibu Waziri wa Nishati, Steven Byabato ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutoa mafunzo maalum ya mara kwa mara kwa vitengo vya kutoa huduma kwa wateja ili kuboresha utendaji kazi wa vitengo hivyo na kutoa huduma bora kwa wateja.
Byabato alisema hayo wakati wa mkutano wake na wafanyakazi wa Shirika hilo mkoani Manyara wenye wenye lengo la kufahamiana, kusikiliza changamoto zinazowakabili pamoja na kutoa maelekezo ya kuboresha utendaji kazi wa shirika hilo uliofanyika Februari 17, 2021 mkoani humo.
Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine, alisema kuwa vitengo vya kutoa huduma kwa wateja vimekuwa vikiongoza kwa kulalamikiwa na wateja kwa kutoa lugha isiyofaa na wakati mwingine hata kutosikiliza wateja jambo linaloleta dosari TANESCO.
Aidha aliutaka uongozi wa TANESCO mkoani Manyara kujipanga na kutoka mafunzo kwa watumishi wake wa vitengo hivyo ya namna ya kuwa na lugha nzuri kwa wateja, kuwaelewesha wateja pale inapotekea changamoto, pindi wanawahudumia.
Aliweka wazi kuwa watuoa huduma kwa wateja katika Mkoa wa Manyara huo wamekuwa wakilalamikiwa sana na wateja jambo linaloleta dosari watumishi wote wa Mkoa huo.
Watumishi wa TANESCO msikubali watu wachache wakaharibu sifa ya shirika lenu ya kutoa huduma kwa wananchi, ninyi mmesambaa nchi nzima, hakikisheni mtoa mafunzo ya mara kwa mara katika vitengo hivi maana ndiyo kilio kikubwa kwa wateja, na mkiona mtu habadiliki basi mu,mumuonye na ikishindikana aondolewe kabisa”, alisema Byabato.
Sambasamba na hilo aliwataka watoa numba za kulipia huduma ya umeme pamoja na watathmini ( Surveyor) kubadilika na kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na taaluma zao kwa kuwa wamekuwa wakilalamikiwa sana kwa kuchelewa kutekeleza majukumu yao kwa wakati na hivyo kuleta sifa mbaya kwa TANESCO.
Vilevile alitoa onyo kwa watumishi kuwa mahusiano ya kimapenzi sehemu za kazi kwa kuwa huharibu utendaji kazi, na kusabibisha watumishi hao kufanya kazi bila kuzingatia weledi na taaluma zao za kazi.
Alisema kuwa endapo watumishi wamependana katika eneo la kazi, wahalalishe mahusiano yao kwa kukufunga ndoa na baada ya hapo wanandoa hao kutenganishwa kutoka ofisi moja kwenda nyingine kwa maslahi ya ofisi husika na familia hiyo.
Kwa wale watakaobainika kuwa na mahusiano, kutoyaweka wazi kwa kuhalalisha, wakaharibu kazi kutokana na mahusiano yao, wachukuliwe hatua za kinidhmu.
Hatutavumilia kuona kazi nzuri iliyofanywa kwa muda mrefu ikaharibiwa na watu wachache kwa kuwa tu ni wapenzi, unakuta mtu ana mahusiano na mwenzake hapo ofisini, wakija wateja atawahudumia tofauti ili mtu huyo aondoke, amlinde Mapenzi wake!hii hatutakubali mteja apate huduma mbaya, tukibaini tutakuondoa wewe kazini”, alisema Byabato.
Aliziagiza ofisi zote za TANESCO kote nchini, kuweka utaratibu wa kuwa na vikao vya mara kwa mara na watumishi wake katika kila idara na Vitengo, kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa hadi kanda ili kuweza kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyakazi wake na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati.
Alisema kuwa kwa kufanya hivyo kutawaweka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa kasi zaidi, ubunifu mkubwa na usahihi pia kutaongeza ari ya kufanya kazi.
Aidha aliwataka watumishi wote kufanya kazi kwa kuheshimiana na kushirikiana kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu kwa kuwa watumishi wote wanategemeana katika utendaji kazi wao.
Katika mkutano huo aliwataka watumishi wa TANESCO, kufanya kazi kwa kasi, ubunifu na kwa usahihi kama kauli mbiu ya Wizara ya Nishati inayoelekeza kwa wafanyakazi wote wa wizara hiyo na taasisi zilizochini yake.
Katika hatua nyingine, mara baada ya kumaliza mkutano na watumishi hao, akiwa njiani kuelekea Jijini Dodoma, Naibu Waziri huyo aliwasha umeme katika Mtaa wa Kandaka, Kata ya Bonga katika Halmashauri ya Mji wa Babati mkoani Manyara.