Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James akiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti wakisaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma Katika ni Mwanasheria wa Wizara ya Fedha Bi.Loveness Msechu akishuhudia.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James akiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti wakionyesha mikataba mara baada ya Serikali kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James akipongezana na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti mara baada ya kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James ,akizungumza mara baada ya kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Baadhi ya Makatibu wakuu kutoka wizara mbalimbali wakifatilia utiaji saini wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti ,akizungumza mara baada ya kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 kwa Kuipa Tanzania fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdeo ,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce Nzuki,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi.Amina Shaaban ,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James ,akiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti hafla iliyofanyika leo Februari 16,2021 Jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imesaini mikataba ya fedha chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Sh Bilioni 307.9 fedha ambazo zitatekelezwa katika miradi sita tofauti ikiwa ni sehemu ya mpango wa ushirikiano wa 11 chini ya mfuko wa maendeleo wa Ulaya.
Hayo yamesemwa leo Februari 16,2021 jijini Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James baada ya kusaini mikataba hiyo ambapo amesema fedha hizo zitaelekezwa kwenye miradi hiyo sita.
Ameitajaa miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa kwanza ni wa kuboresha sekta ya Nishati,jumla ya gharama za kutekeleza mradi huu ni Euro mil.35ambapo ni sawa na bil.96.7.
“Lengo kuu la mradi huu ni kuendeleza sekta ya nishati nchini Tanzania,pia mradi huu unakusudia kuboresha utoaji wa huduma na thamani ya huduma kwa wateja wa shirika la umeme nchini (TANESCO),upatikanaji wa nishati safi, mazingira mazuri ya biashara na kuboreshwa kwa sera ya nishati ili keleta tija na ufanisi,nakuimarisha maarifa na uchambuzi wa taarifa za nishati.
Pia amesema kuwa kuimarisha maarifa na uchambuzi wa taarifa za nishati pamoja na kuanzishwa kwa kanzidata ya masuala ya nishati kwaajili ya mipango na maamuzi.
Mradi wa Pili amesema kuwa niwa matumizi endelevu ya nishati ya kupikia,jumla ya gharama za mradi huu ni Euro mil.30 ambapo ni sawa n ash.bil 82.8.
“Lengo kuu la mradi huu ni kupunguza madhara yanayosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi hapa nchini,lakini pia mradi huu unakusudia kusaidia uzalishaji endelevu wa nishati itokanayo na miti,na kuboresha matumizi bora ya nishati itokanayo na miti sambamba na kuongeza matumizi ya nishati ya kisasa na bora kwa maeneo ya mijini”amesema James.
Ametaja mradi wa tatu kuwa nikusaidia mnyororo wa thamani mnyororo wa thamani katika ufugaji nyuki ambapo gharama zake ni Euro mil.10,sawa n ash. Bil.27.6.
“Lengo kuu la mradi huo ni kuimarisha mchango wa sekta ya ufugaji nyuki katika kukuza uchumi nchini Tanzania,na mradi huu unakusudia kuhakikisha upatikanaji wa asali yenye ubora inayozalishwa katika mazingira mazuri ili kuchochea soko la asali inayozalishwa nchini”amesema.
Aidha mardi mwingine ni kuboresha huduma ya afya ya mimea nchini ili kuongeza usalama wa chakula,ambapo mradi huo utagharimu kiasi cha Euro mil.10 sawa n bil.27.6.
Bw.James amesema kuwa lengo kuu la mradi huu ni kuongeza upatiakanaji wa mazao salama na bora ya kilimo kwa masoko ya kitaifa na kimataifa.
“Mradi huu unakusudia kuhakikisha mfumo wa kitaifa wa udhibiti uingizaji na zinazotoa huduma za afya ya mimea zinatumia mfumo sahihi wa ufuatiliaji na usimamizi”amesisitiza.
Pia alisema kuwa mradi mwingine wa tano ni kusaidia kuboresha mazingiraya biashara ukuaji na ubunifu,nakusema kuwa gharama za kutekeleza mradi huo ni Euro mil23 sawa na sh.bil 63.5.
“Lengo la maradi huu ni kuimarisha mazingira ya biashara kwenye mifumo ya leseni,vibali,kanuni na tozo mbalimbali kama ilivyoainishwa kwwenye mpango wa kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini ambao pia unalenga kuimarisha taasisi ya viwango (TBS) kwa kuipatia vifaa na kuboresha mifumo yake ili kuweza kutekeleza majuku yake kikamilifu”alisema James.
Vile vile Katibu huyo aliutaja maradi wa sita kuwa ni ushirikiano wa kitaalam mabapo gharama za mradi huo ni Euro mil.3.5 sawa na sh.bil.9.7,aidha alisem,a lengo la mradi huo ni kuwezesha Tanzania kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kupitia ushirikiano wa EU NA Tanzania.
“Mradi huu unakusudia kusaidia ukamilishaji wa miradi inayoendelea kutekelezwa kupitia mpango wa 11 wa EDF,na kusaidia serikali ya Tanzania katika uandaaji wa miradi mipya itakayofadhiliwa kupitia mpango ujao wa ushirikiano kwa kipindi cha 2021-2027”alisema.
Wakati huohuo Katibu Mkuu huyo alisema anaushukuru umoja wa ulaya kwa misaada yak e kwa Tanzania kwani imekuja kwa wakati muafaka ambapo serikali inaweka mazingira wezeshi ya kukuza viwanda kwaajili ya ukuaji wa uchumi wetu.
Alisema kuwa mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka mitano(FYDP)ambao upo katika maandalizi pamoja na dira ya maendeleo 2050 iliyoidhinishwa hivi karibuni kw upande wa Zanzibar ni nyenzo muhimu katika uandaaji wa mapango ujao wa ushirikino wa maendeleo baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya.
Kwa upande wqke ,Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini,Manfred Fanti amesema lengo lao ni kuhakikisha bidhaa za hapa nchini zinapata soko Ulaya huku akisisitiza umuhimu wa bidhaa hizo kuongezwa thamani.
Naye,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Dk.Aloyce Nzuki amesema kuwa Wizara yake inayofuraha kupata miradi miwili ambayo ni wa matumizi endelevu ya nishati ya kupikia pamoja na ule wa kusaidia mnyororo wa thamani katika ufugaji nyuki.
Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara,Profesa Riziki Shemdoe aliishukuru (EU) kwa miradi hiyo ambapo aliahidi Serikali ya Tanzania kuisimamia vizuri.