Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhandisi Omari Juma Kipanga akimsikiliza mkandarasi anayekarabati miundombinu ya majengo ya Chuo cha Ulimu Shinyanga Bw.Thadeus Koyanga alipofika Chuoni hapo jana kujionea ukarabati wa miundombinu hiyo.Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Yasinta Mboneko.
Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhandisi Omari Juma Kipanga akifanya ukaguzi wa ukarabati wa miundombinu ya majengo ya Chuo cha Ulimu Shinyanga alipofika Chuoni hapo jana kujionea ukarabati wa miundombinu hiyo.Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Yasinta Mboneko.
Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhandisi Omari Juma Kipanga akiwasiliana na Meneja Mauzo wa Kamuni ya ALAF ili aweze kuwasilisha bati kwa haraka katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buangija Shinyanga Bw.Thadeus Koyanga alipofika Chuoni hapo jana kujionea ukarabati wa miundombinu hiyo.
Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhandisi Omari Juma Kipanga akiwa tayari kuanza ukaguzi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA Wilayani Kishapu jana.
……………………………………………………………………………………
Na Mwansishi wetu-Shinyanga
Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhandisi Omari Juma Kipanga amemtaka mkandarasi anayekarabati miundombinu ya majengo ya Chuo cha Ulimu Shinyanga kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo ifikapo Machi 31, mwaka huu kabla ya wanachuo walioko katika mafunzo kwa vitendo hawajaanza muhula mpya wa masomo.
Naibu Waziri Kipanga alitoa agizo hilo wakati wa ziara ya ziku moja Mkoani Shinyanga kujionea maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Veta Kishapu, Ukarabati wa Miundombinu ya Majengo ya Chuo Cha Uhalimu Shinyanga na Ujenzi wa Madarasa na Mabweni wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Buangija.
Aidha Naibu Waziri Kipanga alishangazwa na hatua ya mkandarasi huyo kufanya kazi yake kwa muda mrefu na kuongeza kuwa kandarasi inapochukua muda mrefu bila kukamilika matokeo yake mkandarasi anakuwa anafanya kazi kwa hasara jambo ambalo linasababisha mkandarasa kushindwa kukamilisha kazi yake.
Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri huyo alijionea namna gani msimamizi wa mradi huo alivyoshindwa kusimamia vyema mradi huo na kutishia kumfukuza katika kazi hiyo baada kujionea baadhi ya mapungufu katika maendeleo ya ujenzi huo.
Aidha alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Yasinta Mboneko kuhakikisha anatembelea mradi wa ukarabati wa ujenzi wa miundombinu ya Chuo hicho kila wiki ili kuhakikisha mkandarasi anakamilisha kazi hiyo kwa wakati na kutoa taarifa kwa Wizara yake kama mapungufu yaliyoko yataendelea kujitokeza.
Katika Ziara yakae hiyo Naibu Waziri Kipanga pia alitambelea mradi Mkubwa ujenzi wa Chuo Cha Ufundi VETA unaoendelea Wilayani Kishapu ambapo pia alijionea kasoro mbalimbali na kuagiza kufanyika kwa marekebisho yaliyopo lakini pia kuhakikisha pesa zilizotengwa kwa jili ya mradi huo zinatosha kukamilisha ujenzi wa Chuo hicho.
Akiongea mbele ya Naibu Wazri huyo Mkurugenzi wa VETA Nchini Bw. Pancras Bujura alisema serikali imetenga kiasi cha Tsh. Bil.1.6 kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho na tayari fedha ambazo zimekwisha tumika ni kiasi cha Tsh. Bil.1.2.
Aidha Baada ya Naibu Waziri kutembelea majengo ya Chuo hicho alionekana kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho na kumtaka msamamizi wa ujenzi wa Chuo hicho ambaye ni VETA Tanzania kuhakikisha natumia kiasi cha fedha kilichabaki kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi wa Chuo hicho.
Kiasi cha fedha kilichobaki katika ujenzi wa Chuo hicho ni takribani Tsh. milioni 400 kiwango ambacho kilitia shaka kwa Naibu Waziri huyo kuwa kuna wasiwasi huenda kiasi hicho cha fedha uenda kisikamilishe ujenzi wa chuo hicho kukubwa hapa Nchini.
Naibu Waziri Omari Juma Kipanga tayari amekamilisha ziara yake Mkoani Shinyanga na anaendelea na Ziara kama hiyo katika mikoa mingine kwa ajili ya kujionea ujenzi wa miundombinu ya Shule ikiwemo masuala mengine ya elimu hapa Nchini.