Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

0

………………………………………………………………………….

MSAKO MKALI WA KATA KWA KATA KWA LENGO LA KUZUIA VITENDO VYA KIHALIFU NA KUKAMATA WAHALIFU NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEFANYA MSAKO MKALI KUANZIA JANUARI – FEBRUARI 16  2021 NA KUFANIKIWA KUKAMATA WATUHUMIWA 17 WA MAKOSA MBALIMBALI NA VITU VILIVYOPORWA VIKIWEMO LUNINGA, SIMU ZA MKONONI, PIKIPIKI, MADAWA YA KULEVYA, PIA  MITAMBO YA KUTENGENEZEA POMBE HARAMU YA MOSHI  IMEKAMATWA.

KUFUATIA MSAKO HUO PIA WAMEKAMATWA VINARA WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA MAUAJI KWENYE FAMILIA, MAKOSA YA  UKATILI  WA KIJINSIA PAMOJA NA UBAKAJI, WATUHUMIWA WOTE  HAWA USHAHIDI UMEKAMILIKA KWA KIWANGO KIKUBWA NA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO.

 1. MTUHUMIWA SUGU WA MAUAJI: –

-BAKARI HAMISI, MIAKA 21, MSUKUMA, MLIMANI “B”. AMAHUSIKA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI YA MAUAJI.

 1. WATUHUMIWA SUGU WAMAKOSA YA UVUNJAJI:-
 • JOHN EZEKIEL, MIAKA 25, MSUKUMA, KAYENZE, MKULIMA.
 • AMOSI LUCAS, MKEREWE, MIAKA 19, MKULIMA, KAYENZE.
 • DANIEL MUSSA, MIAKA 24, MSUKUMA, MKULIMA, KAYENZE.
 1. WATUHUMIWA SUGU WA MAKOSA YA UBAKAJI:-
 • SAID YUSUFU, MIAKA 24, MUHA, MWANAFUNZI.
 • SAID RAMADHANI, MIAKA 27, MSUKUMA, BUSWELU.
 • PASCHAL BONIFACE, MIAKA 47, MJITA, MWAKARUNDI.
 • HAMIS HUSSEN, MIAKA 60, MUHA, MVUVI, KIRUMBA.
 • SHABAN SAREHE, MIAKA 9, MSUKUMA, BEZI.

 1. VITU MBALIMBALI VILIVYOKAMATWA:-

GARI NO.T121 DHE AINA YA TOYOTA HARRIER AMBALO LIMEWEKEWA CHESSIS NA NAMBA ZA USAJIRI WA GARI NYINGINE, PIKIPIKI 6, LUNINGA 10 FLAT SCREEN,  SUBOUFER 4, SIMU ZA MKONONI 51 ZA AINA MBALIMBALI, MITAMBO 7 YA KUTENGENEZEA POMBE HARAMU YA MOSHI, POMBE YA MOSHI LITA 100, BHANGI KILOGRAMU 100, MIRUNGI KILOGRAM 30  NA CUMPUTER 2 (DESK TOP).

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA KUWASHUKURU WANANCHI KWA USHIRIKIANO MZURI. PIA KUSISITIZA WASIFUMBIE MACHO VITENDO VYA UHALIFU BALI WAENDELEE KUTOA TAARIFA ILI ZIWEZE KUFANYIWA KAZI KWA HARAKA NA KUFANYA MKOA WA MWANZA KUWA SALAMA. WANUNUZI WA VYOMBO VYA MOTO WANASHAURIWA KUJIRIDHISHA TRA KABLA YA KUFANYA MANUNUZI VIVYO HIVYO NA KWENYE UNUNUZI WA ARDHI KAMA VIWANJA NA MASHAMBA KABLA YA MANUNUZI WASHIRIKISHE MAMLAKA ZOTE HUSIKA ZA ARDHI ILI KUEPUSHA UTAPELI NA KUIBIWA PESA.