Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiangalia viatu wakati alipotembelea banda la International Leather Industries Co. Ltd) lililopo Katika maonesho ya nne ya programu ya uwezeshaji kiuchumi wananchi yanayofanyika Katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Fredrick Njoka afisa uhusiano wa ambaye pia ni meneja Masoko wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro (Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd) akitoa maelekezo ya bidhaa ambazo wanatengeneza kwa wananchi waliotembelea katika banda lao akiwemo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Watanzania wametakiwa kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo bidhaa za viatu zinazozalishwa na kiwanda cha Kilimanjaro kwani vina ubora wa kimataifa .
Hayo yamebainishwa na Fredrick Njoka afisa uhusiano wa ambaye pia ni meneja Masoko wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro (Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd) ambacho kinamilikiwa kwa ubia kati ya PSSSF na Jeshi la Magereza kilichopo mkoani Kilimanjaro alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika banda lao lililopo katika maonyesho ya nne ya mifuko ya programu za uwezeshwaji wananchi kiuchumi yanayoendelea mkoani Arusha.
Alisema watanzania wanatakiwa kujua kuwa wanaposema Tanzania ya viwanda ni lazima waanze kupenda na kuunga mkono vitu na bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vya hapa nyumbani,pia tuhamasishane watanzania wenyewe kwa wenyewe kupenda vitu vya ndani.
Alisema kuwa kiwanda hicho kimesaidia upatikana kwa soko la uhakika la ngozi ghafi kutoka kwa wafugaji, Kuongezeka thamani ya ngozi inayozalishwa hapa nchini kutokana na mpango wa mafunzo maalumu kwa wafugaji na ajira za moja kwa moja 3000 na zaidi ya ajira 7000 zisizo za moja kwa moja katika mnyororo wa thamani na huduma.
Alisema kiwanda hichi kinasaidia Kuongeza mapato kwa Taifa kupitia kodi mbalimbali, pia kina manufaa makubwa kwa mkoa wa Kilimanjaro pamoja na mikoa jirani kwa kuboresha mfumo wa maisha na kuongeza kipato kwa wakazi, majengo na miundombinu na kinaokoa fedha za kigeni kwa kupunguza uingizaji wa bidhaa za ngozi nchini na kuongeza mapato ya fedha za kigeni kwa kuuza bidhaa za ngozi nje ya nchi.
Alisema kuwanzishwa kwa Kiwanda hiki cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro kumekuwa na manufaa mengi kwa Taifa ikiwemo kuzalisha ajira nyingi kwa wananchi, kupunguza matumizi ya fedha za kigeni pamoja na kuongeza wigo na thamani ya soko la ngozi kwa wafugaji
Alibainisha kuwa kiwanda hichi kinatengeneza soli za viatu jozi 2.1 na bidhaa mbalimbali za ngozi kama vile Mikanda, Mabegi, Pochi, Mikoba na Majaketi ngozi zenye ubora wa kimataifa na ubora wa uhakika ambapo alisema bidhaa zote wanazitengeneza kwa bidhaa halisi ya ngozi za ng’ombe na mbuzi wa hapa nchini.
“Watanzania waache kuvaa bidhaa za mtumba plastic kwani bidhaa Kama za mtumba na za plastic zinamathara makubwa Sana na zinaweza kuletea mtu mathara unaweza unakuta unavaa kiatu Cha mtumba mtu alievaa huko kilipotoka labda alikuwa na fangasi ukivaa na wewe unapata fangasi ,Sasa kuliko yote hayo bora tujijengee tabia ya kuvaa viatu vipya vya ngozi ambapo tunabahati maana tunakiwanda ambacho kinatengeneza viatu hivi hapa hapa nchini”alibainisha Njoka.