Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Dodoma Meja Msitaafu Johnick salingo akizungumza jambo wakati wa ziara ya kamati ya siasa kutembelea katika maeneo ya barabara korofi ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi kuwa hazipitiki katika Jiji la Dodoma.
Meneja wa Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA Mhandisi Godlack Mbanga akitoleo ufafanuzi wa jambo kwa kamati ya siasa ya Wilaya ya Dodoma walipofanyaziara kukagua miundombinu ya barabara katika jiji la Dodoma.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Dodoma Bi Diana Madakwa akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya siasa kutembelea kukagua miondombinu ya barabara katika jiji la Dodoma.
Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Dodoma ikiwa katika maeneo tofauti wakati wa ziara ya kukagua miondombinu ya barabara katika jiji la Dodoma.
…………………………………………………………………………………………..
Na.Ezekiel Mtonyole,Dodoma
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Dodoma imekuja na njia mpya ya kuhakikisha huduma ya miondombinu ya usafiri inaboreshwa kwa kufanya ziara na Wakala wa barabara za Mjini na vijijini TARURA katika maeneo yote korofi yanayolalamikiwa na wananchi kutopitika hasa katika kipindi hiki cha mvua.
Ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kamati ya siasa kukagua miradi na huduma za kijamii imetembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma ambayo miondombinu yake si rafiki kwa watumiaji kutokana na kuharibika vibaya.
Kamati imepita na kukagua barabara ya Ihumwa inayounganisha barabara kuu ya Morogoro na stesheni ya treni ya kisasa inayojengwa katika eneo la Ihumwa barabara ambayo imeharibika kutokana na kutumika na magari makubwa yanayofikisha vifaa vya ujenzi katika stesheni ya Treni.
Barabara nyingine ni barabara za kata ya Nzuguni ambazo baadhi yake zinalalamikiwa na wananchi kutopitika kabisa kutokana na ubovu, barabara za kata ya kilimani katika eneo la Chinyoya ambazo pia hazipitiki, barabara za kata ya Kikuyu na baadhi ya barabara katika eneo la Mtaa wa Area C.
Ambapo Meneja wa TARURA Wilaya ya Dodoma Mhandisi Godlack Mbanga amesema TARURA imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha barabara zote katika Jiji la Dodoma zinapitika huku akibainisha kuwa changamoto ni baadhi ya barabara kutokusajiliwa hivyo kukosa bajeti lakini wamekuwa wakishirikiana na Jiji la Dodoma katika kuziboresha.
“Barabara nyingi zinaendelea kukarabatiwa na nyingine tayari wakandarasi wamesha saini mikataba tayari kwa ujenzi, changamoto ni baadhi ya barabara hazijasajiliwa lakini tunashirikiana na jiji kwa wao kutoa vifaa na sisi kuchangia mafuta ili barabara zote zikarabatiwe” amesema Mbanga.