Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa wanafunzi na walimu wa kike wa VETA alipotembelea maonyesho, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi yanayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.
*********************************************
Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi huadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Februari, 2021 kuhamasisha ushiriki wa wanawake na wasichana kwenye masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hesabu.
Kauli Mbiu ya Siku hii mwaka huu ni, “Mchango wa Wanawake katika Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hesabu katika kufikia Tanzania ya Viwanda.”
VETA imeshiriki kwenye siku hii kama sehemu ya kuendelea kutoa hamasa kwa vijana wa kike kujiunga na masomo ya ufundi stadi hasa kwa kuzingatia kuwa fani nyingi za ufundi stadi zinahusika na sayansi, teknolojia na uhandisi na baadhi ya watu bado wana mtazamo kuwa fani ni za vijana wa kiume.