Home Siasa SPIKA NDUGAI AWAAPISHA WABUNGE WATANO KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI

SPIKA NDUGAI AWAAPISHA WABUNGE WATANO KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI

0

Mwakilishi wa Baraza la wawakilishi, Ameir Abdallah Amir akiapoishwa leo Februari 11,2021 bungeni jijini Dodoma kuwa mbunge

Mwakilishi wa Baraza la wawakilishi, Bakari Hamad Bakari akiapishwa leo Februari 11,2021 bungeni jijini Dodoma

Mwakilishi wa Baraza la wawakiliishi, Bahati Khamis Kombo akiapishwa leo Februari 11,2021 bungeni jijini Dodoma

Mwakilishi wa Baraza la wawakilishi Zanzibar, Mwanatatu Mbaraka Khamis akiapishwa leo Februari 11,2021 bungeni jijini Dodoma

Mwakilishi wa Baraza la wawakilishi Zanzibar , Suleiman Haroub Suleiman akiapishwa leo Februari 11,2021 bungeni jijini Dodoma . Picha zote na Anthony Siame

……………………………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amewaapisha wabunge watano kutoka Baraza la Wawakilishi kuwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ambavyo Katiba inaelekeza.

Wabunge hao ni Amein Abdallah Ameir, Bakari Hamad Bakari, Bahati Khamis Kombo, Mwantatu Mbarak Khamis na Suleiman Haroub Suleiman.

” Leo Wabunge watano wamekula kiapo cha uaminifu baada ya kupokea waraka wa Spika wa Bunge la Wawakilishi Zanzibar, Zuberi Ali Maulid kama ambavyo Katiba yetu inataka wabunge watano kutoka Baraza la Wawakilishi wawe sehemu ya bunge letu,