Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara akizungumza na TV ya Taifa ya Congo amesema ,Simba inawaheshimu Vitta Club na inajua ni timu ngumu mno kucheza nayo kwao kisha kupata matokeo chanya,lakini hatukuja huku kumuogopa mtu!!
Amesema heshma yetu ni ya kimchezo na hatuiangalii historia ya mechi iliyopita ya hapa Kinshasa,
‘Kocha wetu ni mwerevu na atakuja na mbinu sahihi ya kucheza mchezo wa ugenini kama huu” Amemaliza Manara.