***************************************
Na Mwandishi wetu, Hanang’
WAJUMBE wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, chini ya Mwenyekiti wake Comred Mathew Darema, wameendelea na ziara yao ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama sehemu ya maadhimisho miaka ya 44 ya kuzaliwa kwa CCM Tanzania na leo ikiwa ni zamu ya Kata ya Mogitu.
Wakiwa kata ya mogitu wajumbe hao wamekagua na kuridhishwa na maendeleo ya kasi ya miradi hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya, Vyumba vya madarasa na Mradi wa Maji ambao siku chache zijazo utamaliza kabisa changamoto ya upungufu mkubwa wa maji katika mji wa katesh.
Miradi yote imekamilika kwa Asimilia 99% na hivyo kutoa matumaini makubwa kwa wananchi wa Mji wa Katesh na Viunga vyake.
Hongereni sana Viongozi wetu mmedhihirisha kwa Vitendo kwamba CCM ni Chama imara iliyotupa Serikali imara kwa jili ya wananchi wote hasa wanyonge wa Taifa letu.