Kamishna Msaidizi Huduma za Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA Bw.Juma Kuji akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini waliotembelea katika Makao Mkuu ya Shirika hilo jijini Arusha ikiwa ni moja ya mafunzo ya Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App) yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango na kufanyika jijini Arusha kushoto ni Christopher Mtibili Kamishna Msaidizi Mkaguzi wa ndani TANAPA.
Kamishna Masidizi Mwandamizi Tehama TANAPA Bw.Boniface Mariki akizungumza na kutoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App) uliyoleta manufaa kwa TANAPA.
Neema Maregeli Mchumi Mwandamizi Wizara ya Fedha na Mipango akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja.
Kamishna Msaidizi Huduma za Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA Bw.Juma Kuji akimsikiliza Catherine Mbena Afisa Mawasiliano (TANAPA) wakati wahariri wa vyombo vya habari walipofika makao makuu ya hayo kupata uelewa kuhusu Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App) unavyofanya kazi kushoto ni Christopher Mtibili Kamishna Msaidizi Mkaguzi wa ndani TANAPA.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali wakifuatilia maelezo ya Kamishna Msaidizi Huduma za Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA Bw.Juma Kuji wakati akizungumza na wahariri hao walipotembelea katika makao makuu ya shirika hilo jijini Arusha
Baadhi ya Makamishna Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa la TANAPA na Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika kikao hicho.
Mkuu wa Uendeshaji wa Mfumo wa GePG kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Basil Baligumya katikati akitoa ufafanuzi wakati wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea Chuo cha Ufundi Arusha kulia ni Neema Maregeli Mchumi Mwandamizi Wizara ya Fedha na Mipango na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja.
Mkuu wa Uendeshaji wa Mfumo wa GePG kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Basil Baligumya akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja wakifuatilia maelezo ya wataalamu wa mifumo ya fedha Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA wakati wahariri walipotembelea shirika hilo leo.
…………………………………………..
Naibu kamishna Msaidizi Huduma za Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA Bw.Juma Kuji amesema kuwa Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App) Umeongeza uwajibikaji na uwazi katika ukusanyaji mapato pamoja na kuongeza mapato kwa kiwango kikubwa.
Akizungumza na wahariri wa Vyombo vya habari nchini waliofika katika makao makuu ya shirika hilo yaliyopo jijini Arusha,naibu kamishna Msaidizi Huduma za Shirika Juma Kuji alisema kuwa Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App) umeleta manufaa makubwa pamoja na kuboresha muda wa kuhudumia wateja.
Naibu kamishna Kuji alisema kuwa katika makusanyo ambayo yanafanywa na Tanapa katika maeneo ya hifadhi yamewezesha shirika hilo kukusanya kiasi cha shilingi bil.100 hadi 200 kabla ya mfumo huu na kufikia kiasi cha shilingi bil.360 kwa mwaka kabla ya janga la Corona.
“Ndugu zangu wahariri mfumo huu wa GePG tulikuwa na akaunti kama 100 za kukusanya makusanyo kote nchini nah ii ilikuwa inatupa kazi kubwa na gharama kubwa kuandaa ripoti kukusanya taarifa na hata kuzipata fedha zenyewe,pia ilikuwa inatugharimu gharama za benki hizi kwa wingi huu kukosekana kwa uwazi na kazi ngumu ya upatanisho wa kifedha kati ya benki na vitabu tulivyonavyo,ilikuwa ngumu sana”alisema Naibu Kamishna Kuji
Pia alisema kuwa wingi wa akaunti za kuhifadhia fedha umepungua kutoka akaunti 100 hadi kubakia akaunti nane ambapo nne ni za kukusanya fedha za ndani na nne ni za makusanyo ya nje yaani dola.
“Tumepunguza utitiri wa Akaunti zetu kwasababu tuna mageti 8 nchi nzima,kuendesha akaunti 100 ni kazi kubwa kutengeneza taarifa zote hizi ni lazima utafute mhasibu mmoja baada ya nyingine,kuna gharama kubwa zimepungua,hivyo basi tunaweza kuyaona makusanyo yote kwa muda mchache sana na kwa uwazi na gharama zikawa hakuna kabisa,rahisi mno na ripoti inapatikana mara moja”alisema Naibu Kamishna Kuji
Nae Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ukaguzi wa ndani Christopher Mtibili alisema kuwa kupitia mfumo wa GePG umewezesha kuongeza mapato kupitia makusanyo na kuchangia pato la Taifa pia.
Alisema kipindi cha nyuma kabl ya mfumo huu walikuwa wakipata changamoto mbali mbali ambapo chaneli za malipo zilikuwa nyingi,tofauti na sasa ni control namba tu.
Hata hivyo Afisa Mwandamizi Uhifadhi (TEHAMA) Bw.Boniface Mariki alisema kuwa mfumo huo umewawezesha waongoza watalii kuweza kuokoa muda na kuwawezesha kulipa kabla kabla ya kupata huduma na hata kama kuna makosa ya kiufundi basi kupitia mfumo huo yanaweza kurekebishika.
“Wafanyabiashara wengie wengine walikuwa wanataka huduma kwanza kisha kulipa baadae lakini kutokana na mfumo huu huwezi kupata huduma yeyote bila kulipia utalipa kwanza ndio upate huduma maana hakuna mazungumzo hivyo hasara hakuna kabisa,hata mtu akilipa zaidi ya mara moja kupitia mfumo huu unaweza kuona kila kitu na ukaweza kumsaidia”Alisema Afisa Mariki
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) lilianza kutumia mfumo huu wa GePG tangu tarehe mosi September,2018