Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, akieleza umuhimu wa kuhusu matumizi ya Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App), ambao ni pamoja na kuokoa mud awa kufanya malipo kwa mwananchi, katika Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini inayofanyika jijini Arusha.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega, akiwataka Wahariri wa Vyombo vya Habari kuendelea kuwa Wazalendo na kuhakikisha wanatoa taarifa kwa umma kwa ukamilifu kuhusu manufaa ya Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App), wakati wa Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini kuhusu mfumo huo inayofanyika jijini Arusha.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, akiwashukuru Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini kwa kuhudhuria katika Semina ya Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App), wakati wa Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini kuhusu mfumo huo inayofanyika jijini Arusha.
Mchumi Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Neema Maregeli, akieleza historia fupi ya Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App), wakati wa Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini kuhusu mfumo huo inayofanyika jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari vinavyofanya kazi na Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwang’onda, akiishukuru Wizara kwa kufanyakazi kwa karibu na Vyombo hivyo, wakati wa Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini kuhusu mfumo huo inayofanyika jijini Arusha.
Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari nchini wakiwa katika Semina ya Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App), jijini Arusha.
Mtaalamu wa Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App), Bw. Basil Baligumya, akitoa elimu kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, wakati wa semina ya mfumo huo, jijini Arusha.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati) akipeana mkono na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, baada ya kufungua semina ya Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App), jijini Arusha. Katikati ni Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati), Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi na Mwenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari vinavyofanya kazi na Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwang’onda, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati), Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi na Mwenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari vinavyofanya kazi na Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwang’onda, wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mfumo wa kulipia malipo ya Serikali kwa kutumia control number ujulikanao kama Government Electronic Payment Gateway (GePG App), jijini Arusha.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati), Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi na Mwenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari vinavyofanya kazi na Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwang’onda, wakiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya uandaaji wa Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
(Picha na Peter Haule, WFM, Arusha)
**************************************
Na. Peter Haule na Ramadhani Kissimba, WFM, Arusha
KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega ameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango na Serikali kwa ujumla kwa kuweka mfumo imara wa ukusanyaji mapato ya Serikali wa GePG ambao unawawezesha wananchi kulipia huduma mbalimbali za Serikali kupitia mfumo huo.
Akizungumza wakati akifungua semina ya siku mbili kwa Wahariri kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari nchini kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, iliyoanza leo jijini Arusha, amesema kuwa mfumo wa GePG umeimarisha ukusanyaji mapato ya ndani na kuwezesha mwananchi kuwa na uhakika wa malipo mbali mbali yanayofanyika kupitia ( Control Number) ambayo ni salama zaidi katika mchakato wa ukusanyaji mapato.
Amesema, mfumo huo pia unawezesha wananchi kuokoa muda kuanzia anapopata Ankara zake, namna ya ulipaji wake, na upatikanaji wa Stakabadhi yake ikiwa ni pamoja na fedha kufika Serikalini kwa wakati na kuepuka upotevu wa mapato ya Serikali.
’’Mfumo huu wa GePG umeimarisha ukusanyaji mapato kwa kuondoa gharama za miamala ya fedha kwa Umma, utaratibu usio rafiki wa ulipaji huduma za Umma pamoja na makusanyo yote kuonekana kwa uwazi na uhakika wa taarifa mbali mbali.” Amesema Kwitega.
Aidha, alisema kuwa, mfumo huu umeweza kuongeza mapato mfano Wakala wa misitu Tanzania walikuwa wakikusanya kiasi cha shilingi bilioni 95 kwa mwaka kabla ya mfumo huu wa GePG lakini baada ya kutumia mfumo huo waliweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni.115.
Vile vile, alisema kuwa Shirika la Umeme TANESCO liliweza kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 38 kwa mwwaka ambazo zilikuwa zikitumika kulipia gharama za wakala kabla ya mfumo huo ambapo baada ya kufunga mfumo huu wameweza kuokoa fedha hizo ambazo zilikuwa gharama za miamala kwa umma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Sausi amewataka wahariri kuhakikisha kuwa wanatoa elimu sahihi kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato(GePG) katika kufanya malipo ya huduma mbalimbali za Serikali . Sausi amesema, kabla ya mfumo huo wa GePG kulikuwa na upotevu mkubwa wa mapato ya Serikali kutokana na kutokuwepo kwa uwazi wa ukusanyaji wa mapato pamoja na ukosefu wa taarifa sahihi na kwa wakati.
“Niwaombe wahariri muwaeleze wananchi kuepuka kulipa pesa taslimu kwa kuwa, kwanza hazitafika kwa wakati pili zitapotea na mwananchi ataingia hasara ya kulipa kwa mara nyingine tena, hivyo watumie ‘Contorl Number’ ili kuepuka upotevu usio wa lazima.”amesema John.
Aidha alisema kuwa Mfumo huo umeunganishwa na Taasisi mbalimbali za Serikali za mitaa, Halmashauri, Taasisi na serikali kuu zipatazo 670.
Bw. Sausi alisema mfumo huo ulianzishwa rasmi mwaka 2017 kwa Taasisi chache ambapo umewezesha kuongezeka kwa mapato kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Mchumi Mwandamizi anayesimamia mapato ya Serikali kutoka Idara ya Uchambuzi wa Sera Bi. Neema Maregeli alibainisha kuwa mfumo wa GePG umeongeza mapato ya Serikali kutoka wastani wa shilingi bilioni 800 kabla ya Mfumo huu hadi wastani wa trioni 2.4 kwa mwaka.
Alisema kuwa mapato haya yamewezesha Serikali kutekeleza shughuli zake mbalimbali ikiwemo kuimarisha utoaji wa huduma kwa jamii na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Vile vile , alisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kupitia wahariri walioshiriki mafunzo hayo kuwaelimisha wananchi kwa ufasaha umuhimu wa kulipa kodi, kudai risiti wanapofanya manunuzi na kwa upande wa wafanya biashara kutoa risiti wanapouza huduma na bidhaa mbalimbali.