************************************************
WAFANYABISHARA ndogondogo wanaofanya biashara ndogondogo eneo la kariakoo Jijini Dar es salaam maarufu kama WAMACHINGA wameiomba Serikali kuwawekea mfumo wa uongozi wa kuchaguliwa na wamachinga wenyewe ili kuweza kuwatatulia kero zao kwa urahisi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo msemaji wa muda wa wamachinga wa karikoo Masud Chauka alisema uongozi uliopo kwa sasa ni batili kutokana na kutokuwa rasmi katika utendaji wa kazi.
Amesema mfumo uliopo kwa sasa sio rafiki kwa wamachinga hivyo upo umuhimu kwa kuwa na viongozi halali waliochaguliwa kwa mujibu wa katiba ya Chama cha wamachinga kariakoo(TAWASO) ambao unaozingatia katiba ya Chama hicho.
” Wamachinga wote wanaofanya biashara ndogo ndogo nchi nzima wanapaswa kutegeneza mfumo wa kuwa wa viongozi wa kuchaguliwa na kupigiwa kura na kuwa na ukomo wa muda wa kishikilia nyadhifa “amesema Chauka
Chauka ame kuwa lengo la kuwa na viongozi waliochaguliwa na wamachinga wenyewe ni kuimarisha utendaji kazi wa sekta ikue kwa kasi na kukuza uchumi ambao utasaidia kuongeza pato la taifa .
Pia amesema wamachinga wanaiunga mkono Shirikisho la Umoja wa vyama vya Wamachinga Taifa ( SHIUMA) lakini wanaitaji kufanyika kwa marekebisho kwa kuchangua viongozi kuanzia ngazi za wilaya,Mkoa na Taifa pamoja na kuunda shirikisho kwa makubaliano ya pande zote.
Kwa upande wake mmoja wa waasisi wa Chama cha wafamachinga karikoo KAWASO, Rajabu Mahundu amesema mpaka sasa imepita takribani miaka 7 bila ya kuwa na uongozi halali waliochaguliwa kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho
Mahundu ameiomba serikali kupitia Wizara ya nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kuwasaidia kuhamasisha viongozi wa ngazi za juu kuwafata wamachinga ngazi za nchini kusikiliza kero zao.
“Tunaiomba serikali ituangalie sisi wamachinga kuanzia mfumo wa chini kwani tunakabiliwa na chagamoto nyingi zinazoitajika kutatuliwa ..
Uwepo wa viongozi waliochaguliwa na wamachinga utatusaidia kutatua kero zinazotukabili kwa muda mrefu.
Hata hivyo ameipongeza serikali kupitia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kwa kuitisha mkutano na wamachinga wote Tanzania uliofanyika hivi karibuni ambao ulilenga kijadili chagamoto mbalimbali zinazowakabili.
” Kikao kazi Cha hivi karibuni na waziri mkuu Kassim Majaliwa kitakwenda kuzitafutia ufumbuzi kwa kuweza kutusaidia kutukutanisha na sekta za kifedha”amesema Mahundu.
Katika hatua nyingine almeomba wakurungezi na wakuu wa wilaya wote wa Halmashauri kuwaimiza wamachinga kwenye maeneo yao kwenda kuchukia vitambulisho vipya kwa ajili ya kuendelea na kazi zao ili kuchangia pato kwa taifa.