Mwenyekiti wa Kundi la Simba Jamii Tanzania Enterprises (SJTE), aliyemaliza muda wake, Gabriel Ntole akizungumza na wanachama wa Kundi hilo pichani hawapo, kushoto ni Mlezi wa SJTE, Hassan Mbilili na Kulia ni Mjumbe kwa Kamati Tendaji James Tindi.
Wanachama wa Kundi la Simba Jamii Tanzania Enterprises (SJTE), wakimsikiliza Mwenyekiti aliyemaliza muda wake SJTE Gabriel Ntole pichani hayupo.
,,..,..,,.,.,..,….,….,,,..,…,…..
NA SULEIMAN MSUYA
WANACHAMA wa Kundi la Simba Jamii Tanzania Enterprises (SJTE), wametakiwa kushikamana na kushirikiana ili kuhakikisha kundi hilo linadumu na kuwa endelevu.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti SJTE aliyemaliza muda wake, Gabriel Ntole wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu na uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Ntole amesema makundi au taasisi mbalimbali zinazohuisisha jamii yamekuwa yakifunjika kutokana na kukosekana kwa mshikamano na ushirikiano baina ya wana kikundi.
Amesema msingi wa mshikamano na ushirikiano unaweza kufanikiwa iwapo viongozi watakuwa wavumilivu na kutunza ndimi zao.
“Kundi hili ni kubwa na linafahamila kila mahali Serikalini hivyo wapo kati yetu wanaona wivu na wengine wametoka hali ambayo inachangia majungu yasiyo na sababu.
Rai yangu ni nyie viongozi kujiepusha na majungu hayo ili kuijenga SJTE yenye nguvu na mafanikio tele,” amesema.
Mwenyekiti amesema kila mwanachama anapaswa kuipigania SJTE kwa nguvu zote ili iendelee kuwa taasisi kubwa na yenye tija kwa nchi.
Aidha, Ntole amewataka wana SJTE kuhakikisha wanafanya uchaguzi wa viongozi kwa kuzingatia sifa ambazo zitawasaidia kuipeleka mbele na sio kuendekeza majungu.
Kwa upande wake Mlezi wa SJTE, Hassan Mbilili aliwataka wana kikundi kuacha kutumia muda mwingi kuendekeza majungu kwani hayana faida na kundi.
Mbilili amewashauri wana SJTE kutumia kundi hilo kutafuta fursa mbalimbali na sio kuendekeza umbea ambao hauna faida.
“Mimi ni moja ya waanzilishi wa kundi hili tumepitia mengi ila hatujakata tamaa naomba viongozi wapya mjipange na kukabiliana na changamoto zote zitakazokuja,” amesema