WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa kwenye kiwanda cha Ihemi kilichopo mkoani Iringa kinachomilikiwa na chama cha mapinduzi akiangalia namna mafundi wanavyoshona nguo mbalimbali
Mkurugenzi wa kampuni ya Asas na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (MNEC) Salim Abri Asas akiwa kwenye moja ya mikutano ya ndani ya chama cha mapinduzi
……………………………………………………………………………..
Na Fredy mgunda,Iringa.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amempongeza mkururugenzi wa kampuni ya Asas Salim Abri Asas kwa jitihada zake za kuleta maendeleo mkoani Iringa kwenye sekta mbalimbali.
Akiwa kwenye ziara ya kukagua mradi wa chuo cha Ihemi na kiwanda cha Ihemi vinavyomikiwa na chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa, mheshimiwa waziri mkuu alisema kuwa kila akienda kukagua miradi ya maendeleo mkoani Iringa lazima akutane na mchango wa Salim Abri Asas katika mradi huo.
Alisema kuwa mkurugenzi huyo wa kampuni ya Asas na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (MNEC) amekuwa akitolea kusaidia kukuza maendeleo ya mkoa wa Iringa kwa ujumla.
Mheshimiwa waziri mkuu alisema kuwa mchango wa MNEC Salim Abri Asas katika chuo cha Ihemi ni mkubwa sana unapaswa kuheshimiwa kweli kweli maana kujitolea kujenga majengo ya chuo na kiwanda sio jambo ambalo linapaswa kupuuzwa kabasi hapa nchini.
Alisema kuwa kwa naiba ya serikali anachukua fursa na kumshukuru na kumpongeza MNEC Salim Abri Asas kwa uchango wake ambao unaongeza ajira n kukuza maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kwa ujumla.
“Kila wakati nikija kwenye ziara mkoani Iringa lazima nikutane na jina la Salim Abri Asas kwenye shughuli za kimaendeleo tena akiwa ametoka mchango unaozidi asilimia zaidi ya themanini hivyo mtu kama huyu anapaswa kuheshimiwa kwa mchango wake “alisema
Akiwa katika kiwanda cha Ihemi waziri mkuu aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuimalisha ulinzi ili kuzitunza Mali zote za kiwanda kutoibiwa tena kama ilivyokuwa hapo awali.
Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi taifa,MWL Raymond Mangwala alishukuru mchango mkubwa uliotewa na MNEC Salim Abri Asas katika haraka za kufanikisha kukifufua chuo na kiwanda cha Ihemi kwani bila mchango wake basi chuo na kiwanda visingekuwa hivyo.
Alisema kuwa kwa asilimia kubwa mashine zinazotumiwa kwenye Kiwanda hicho zimenunuliwa na MNEC Salim Abri Asas na amejenga majengo mengi hapo ukianzia ukumbi madarasa na jengo la kuwa kwa asilimia kubwa ni mchango wa MNEC huyo.
Mangwala alisema kuwa wanachama wa chama cha mapinduzi na wananchi wote wanapaswa kuheshimu na kuthamini mchango wa MNEC Salim Abri Asas kwenye maendeleo ya uchumi katika mkoa wa Iringa.
Nao baadhi ya vijana wa ccm mkoa wa Iringa walimpongeza MNEC Salim Abri Asas kwa kazi kubwa anayoifanya mara kwa mara kuhakikisha chama cha mapinduzi kinaimarika kila siku na kinaongeza wanachama wapya kila uchwao.
Walisema mkoani Iringa kila sekta MNEC Salim Abri Asas amechangia shughuli za kimaendeleo kama vile sekta ya michezo,miundombinu,afya,kilimo,elimu,uwekezaji,mawasiliano,viwanda na kadharika hivyo wananchi wanapaswa kumpa heshima yake.