Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Chengula akiwashukuru wajumbe wa Mamlaka ya Mji huo baada ya kumchagua tena kushika nafasi hiyo.
Wajumbe wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakimsikiliza Mwenyekiti wa mtaa wa Tunduru, Christopher Chengula akiwashukuru baada ya kumchagua tena kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji huo.
…………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu, Mirerani
Mwenyekiti wa mtaa wa Tunduru, Christopher Chengula, amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, baada ya wajumbe kumchagua tena.
Ofisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji huo, Evence Mbogo akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika juzi amesema Chengula alipata kura 32 za wajumbe wote wa mamlaka hiyo kupitia CCM.
Mbogo amesema nafasi ya Makamu Mwenyekiti huwa inashikiliwa kwa kipindi cha mwaka mmoja hivyo uchaguzi huo umefanyika baada ya muhula wa mwaka mmoja kupita.
Mwenyekiti wa mamlaka hiyo, Adam Kobelo amewataja wajumbe wa kamati ya Elimu, Afya na maendeleo ya jamii ni Mwenyekiti Simon Mkumbo, Gadi Msuya, Omary Hussein, Boaz Ambonya, Johari Mwaselela, Omary Onesmo, Josam Lolo, Ochieng Olward, Idd Abdi, Anthony Musiba na Happy Mafie.
Kobelo amewataja wajumbe wa kamati ya huduma za jamii ni Mwenyekiti Juma Selemani, Mweta Singo, Daudi Makala, Atwai Ramadhan, Elifitia Lyimo, Hamad Malya, Happy Msuya, Jacquline Momo, Nalogwa Songelaeli, Abraham Sarakikya, Rajab Msuya na Jema Lilama.
Amewataja wajumbe wa kamati ya Ukimwi ni Mwenyekiti wake Christopher Chengula, Adam Kobelo, Twaha Mpanda, Andrea Nyambo, Ibrahim Mmary, Mary Mdee, Primy Shirima, Joyce Mwasha na Claudia Dengesi.
“Nafasi zangu mbili za upendeleo kwa wajumbe wa kamati ya Fedha ninawateua Joyce Mwasha na Primy Shirima, wataungana na wenyeviti wa kamati nyingine,” amesema Kobelo.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo Chengula amewaahidi wajumbe hao kuwa ataendeleza ushirikiano bila kubagua kata hizo mbili zinazounda mamlaka hiyo.
“Sitaangalia mjumbe ni wa kata ya Mirerani au kata ya Endiamtu wote ni wakwetu tufanyeni kazi kwa kushirikiana kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa eneo letu,” amesema Chengula.
Mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani ilianzishwa mwaka 2008 na hivi sasa ina vitongoji 24 vya kata mbili za Mirerani na Endiamtu, ambavyo vinaunda mamlaka hiyo.