***************************************************************
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy
Hassan Kimanta ameiaigaza mamlaka ya mapatao mkoani humo(TRA) kwa kushirikiana na Tasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwafuatilia watu wote wanaostahili kulipa kodi na kuhakikisha wanalipa.
Kimanta alitoa agizo hilo leo wakatiakifungua kikao Cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) ambalo alisema kuwa ukusanyaji wa kodi ni lazima upewe kipaumbele katikat mkoa huo ili maendeleo yaweze hupatikan katika sekta zote.
Alisema kuwa wakikusanya kodi kwa wingi wanaijengea serikali uwezo wa kutengeneza miundombinu ya vituo vya afya, barabara, maji shule na mengineyo hivyo wale wote wanaostahili kulipa kodi ndani ya mkoa wa Arusha walipe.
“Natoa maelekezo kwa meneja wa TRA mkoa wa Arusha ashirikiane na Kamanda wa TAKUKURU mkoa kuwafuatilia wote wanaostahili kulipa kodi na kuhakikisha wanalipa, tunataka kodi,”Alisema Kimanta.
Alifafanua kuwa hakuna haki bila wajibu hivyo ukusanyaji wa kodi ni lazima kwani ikilipwa wanaijengea serikali uwezo wa kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Aidha kwa upande wa elimu alisema kuwa
elimu mkoa wa Arusha unaongoza kitaifa ambapo katika matokeo ya kidato cha nne na kidato cha pili imeongoza kitaifa huku upande wa afya ukiwa ya pili kwa suala la lishe ikifuatiwa na kigoma.
Alieleza mafanikio hayo yametokana na mshikamano mkubwa walionao unaowafanya wafanikiwe hivyo ni rai yake kuwasihi viongozi wa sekta zote kuendeleza mshikamano huo kwa kuwa wamoja, kupendana ukiwa ni pamojan na pale lenye changamoto kurekebisha kwa haraka.
Alisema katika wilaya zote sita Kuna upungufu wa madarasa 126 ambapo anawashukuru wakuu wa wilaya na wakurugezi kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kuhakikisha ya kujenga madarasa kea kushirikiana na wananchi na hadi kufika February 28 upungufu huo utakuwa umeondoka.
“Lazima madarasa yajengwe na nilazima kasi iongezeke ili pasiwepi na wanafunzi watakaoshindwa kusoma Kutokana na ukosefu wa miundombinu ya madarasa,” Alisema Kimanta.
Aliendelea kusema kuwa mkoa wa Arusha mpaka sasa upo shwari na vyombo vya usalama vinatekeleza wajibu wake kutatua changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza .