Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
mkoani Singida, Justice Kijazi, akizungumza kwenye kikao kazi cha tathmini ya
hali ya matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto wilayani humo jana
kilichoshirikisha wanawake 120 waliokutanishwa na Shirika la SPRF chini ya
ufadhili wa FCS ili kujadili namna bora ya kutokomeza matukio hayo kwa mujibu
wa sheria.
Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Stars of Poverty Rescue Foundation
(SPRF) Dkt. Suleiman Muttani akizungumza
kwenye mkutano huo ulioshirikisha wanawake 120 kutoka vijiji 12 kuzunguka
wilaya ya Ikungi, Singida.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali
zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya
matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali
zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya
matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali
zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya
matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali
zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya
matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.
kazi cha vikundi vya uhamasishaji kwa Sauti Ya Mwanamke na Sauti ya
Mwanafunzi kikiendelea.
Maafisa Watendaji wa Shirika la SPRF wakifuatilia matukio yanayoendelea
kwenye kikao hicho.
la Polisi likishiriki ipasavyo kikao hicho.
Mmoja wa waratibu wa mradi wa Aware, Bernard Maira
akizungumza kwenye kikao hicho.
wa Sauti ya Mwanamke kwenye moja ya makundi ya uhamasishaji akizungumza.
Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ikungi, Beatrice Maeda
akizungumza.
kikiendelea.
ya kikundi cha Uhamasishaji cha Sauti ya Mwanamke wilayani Ikungi
wakieleza moja ya tukio la ukatili wa kijinsia walilofanikiwa kuliibua.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SHIRIKA lisilo la Kiserikali linalojikita zaidi katika
mlengo wa shughuli za kupunguza umaskini kwa afya na ustawi nchini (SPRF)
kupitia mradi wake wa ‘Aware’ jana limewakutanisha
wanawake 120 kutoka vijiji 12 vya wilaya ya Ikungi, mkoani hapa kwa lengo la
kuwaimarisha kuweza kukabiliana ipasavyo na
matukio ya ukatili.
Jumla ya matukio ya
ukatili wa kijinsia 104 yameripotiwa kufanyika ndani ya Wilaya ya Ikungi kwa kipindi cha kati ya Julai 2019 hadi
Novemba 2020, ambapo kati ya matukio hayo 56 yalijitokeza katika kipindi cha
Julai 2019 hadi Februari 2020, huku matukio mengine 48 ya aina hiyo hiyo
yakijitokeza kipindi cha Machi hadi
Novemba 2020.
Kwa mujibu wa SPRF chini ya ufadhili wa Shirika la
Foundation for Civil Society (FCS) imebainika kuwa kati ya matukio hayo 56
yaliyoripotiwa kutoka vijiji 12 vya mradi huo kwa kipindi hicho cha Julai 2019
hadi Februari 2020 ni kesi 2 ndizo zilizofikishwa kwenye ngazi ya mahakama, na
kati ya hizo kesi moja pekee ndiyo iliyotolewa hukumu.
Matukio mengine 7 ya ukatili yaliyoripotiwa yaliishia kwenye
Kituo cha Polisi Ikungi kutokana na kukosa vielelezo na ushahidi shawishi, huku
kesi 4 zikikomea kwenye vituo vidogo vya polisi, 7 kwenye ngazi za kata, 16 ngazi
ya vijiji, 5 ngazi ya vitongoji na 14 zikiishia kutatuliwa kindugu kwenye ngazi
ya familia.
Aidha, kwa upande wa matukio 48 yaliyojitokeza kwenye kipindi cha Machi hadi Novemba 2020 ni
kesi 2 pekee ndizo zilizofikishwa na kuamriwa kwenye ngazi ya mahakama, huku
matukio mengine 11 yakiishia Kituo cha Polisi Ikungi, 5 vituo vidogo vya polisi
kwenye maeneo hayo, 1 ngazi ya kata, 12 vijiji, 6 Ustawi wa Jmii Wilaya, 2
Vitongoji na 7 zikiishia kutatuliwa
kindugu kwenye ngazi ya familia.
Wakichangia ripoti hiyo kabla ya kufikia maazimio, baadhi ya
wanawake kutoka kwenye majukwaa ya Sauti za wanawake na Sauti za Wanafunzi
wilayani hapo walisema bado kuna udhaifu mkubwa katika kushughulikia
utekelezaji wa sheria zinazopinga
vitendo vya ukatili.
“Suala hili limeendelea kuwa sugu na linalochochea ongezeko la matukio ya kufedhehesha, undugu,
ujamaa na urafiki ndio chanzo kikubwa kinachoathiri mwenendo wa mashauri haya
ya ubakaji, ndoa za utotoni na mimba za umri mdogo hasa pale tunaporuhusu
yamalizwe kwenye ngazi za familia,” alisema mmoja wa washiriki wa mkutano huo,
Anna Heneriko.
Mwingine Pili Hussein alisema kesi nyingi zimekuwa
zikimalizwa kwenye ngazi ya vituo vya polisi na kwa maaafisa watendaji. Lakini
kubwa zaidi kuna uvujishaji mkubwa wa siri kwa watoa taarifa jambo ambalo
linafifisha hamasa ya mapambano dhidi ya vitendo hivyo.
Kupitia mkutano huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
hiyo Justice Kijazi aliwataka maafisa wa ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi
kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria katika kuhakikisha mashauri yote
yanayoripotiwa yanafikishwa kwenye ngazi za utatuzi wa kisheria.
“Niwahakikishieni mama zangu wote mliopo hapa serikali yenu
chini ya Rais John Pombe Magufuli ni sikivu sana, na inakwazwa sana na aina
yoyote ya uhalifu na uvunjifu wa sheria kwa makusudi. Nimeguswa sana na matukio
haya yanayofedhehesha mama zetu na watoto wetu…chukueni namba zangu za simu ili
yeyote kati yenu atakayeona tukio lolote la ukatili likitendeka anijulishe,”
alisema Kijazi
Aidha, Kijazi aliwataka aliwataka maafisa Ustawi wa Jamii na
Jeshi la Polisi kuhakikisha wanashughulikia kikamilifu kesi za matukio yote ya
ukatili yanaripotiwa kwa utimilifu unaozingatia matakwa ya kisheria kwa
minajiri ya kutokomeza kabisa vitendo hivyo, sambamba na kuwezesha haki
kuonekana kutendeka.
Hata hivyo, Jeshi la
Polisi Ikungi kupitia mkutano huo liliwataka wananchi wa wilaya hiyo kutoa
ushirikiano wa kutosha pindi matukio hayo yanapojitokeza, na hasa kutoharibu
wala kuwashawishi wahanga kuficha ushahidi ili hatua stahiki za kisheria
zichukuliwe pindi matukio hayo yanapojitokeza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa SPRF, Dkt. Suleiman
Muttani alisema lengo la kikao hicho ni
kutaka kuyaimarisha kiutendaji majukwaa ya vikundi vyote vya uhamasishaji dhidi
ya matukio ya ukatili, ikiwemo kundi la Sauti ya Mwanamke katika kuendelea
kushirikiana na majukwaa mengine kutetea haki za wanawake na watoto.
“Azma ya mradi huu wa ‘Aware’ ni kuona mifumo ya serikali za
mitaa imeimarika kwa kupokea na kuitikia kwa haraka utekelezaji wa mahitaji ya
jamii hasa matakwa ya wanawake, watoto na makundi mengine athirika kuona
wanatambua suala la ukeketaji, ndoa za utotoni, ukatili kwa wanawake na
unyanyasaji kwa watoto haukubaliki,” alisema Muttani
mpaka sasa kati ya matukio yote hayo yaliyoibuliwa kwa
ushirikiano wa majukwaa yake mbalimbali ikiwemo Sauti ya Mwanamke, Sauti ya
Mwanafunzi, Kamati za Mtakuwa na Wanaume Washawishi ndani ya Vitongoji na
Vijiji ni kesi 48 pekee ndizo zilizofika kwenye ngazi za utatuzi huku nyingine
utatuzi wake ukiishia kwenye ngazi za familia.