Mkaguzi wa TBS, kanda ya kusini,Barnabas Jacob akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa soko la Mkuti katika Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, ikiwa ni hatua ya Shirika hilo kutimiza jukumu lake la utoaaji elimu kwa Umma. Wafanyabiashara hao wamesisitizwa kununua na kuuza bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS ili kumlinda mlaji. Pia Afisa Uhusiano Mkuu wa TBS aliwakumbusha wauzaji wa nguo za mitumba katika soko hilo kuendelea kufuata maagizo ya serikali kwa kutokununua na kuuza nguo za ndani za mitumba, ambazo haziruhusiwi kisheria. Kiwango cha nguo za mitumba hakiruhusu uuzwaji wa nguo za ndani za mitumba kama ville sidiria, chupi na nguo za kulalia kwani zinahatarisha usalama wa mtumiaji.